Blog

Kwanini makipa watano katika kikosi cha Stars?

Sambaza....

Mijadala ni mingi juu ya uteuzi wa timu ya Taifa eneo kubwa lilikuwa kutojumuishwa kwa wachezaji Jonas Mkude na Ibrahim Ajibu lakini kuna hoja nyingine ikaibuka kwanini magolikipa watano?

Nikagundua wauliza swali hili “wanasahau” kwamba kikosi hichi  si cha mwisho, kikosi cha wachezaji 23 hakijatajwa! Ambapo kungekuwa na makipa 5 hata mimi ningekuwa wa kwanza kuhoji kwanini makipa 5 kwenye nafasi 23 ? Lakini kwa wakati huu timu bado ina mechi mbili za kirafiki dhid ya wenyeji Misri tarehe 13/6 na ile ya tarehe 16/6 dhidi ya Zimbabwe.

Aishi Manula

Hoja ya msingi hapa kila timu ni lazima isajili wachezaji 23 katika michuano hiyo,na lazima nafasi za makipa ziwe 3 na hii ni kanuni siyo “hiari” sasa basi, Mathalani kocha kaondoka na makipa 3 kwa wakati uliopo kisha golikipa anaumia katika mechi hizi mbili za kwanza kabla ya zile tatu za mashindano unadhani nini kingetokea na kanuni ya usajili imeweka bayana? na kumbuka mwisho wa usajili wa mataifa haya ni 18/6 ,baada ya hapo hakuna usajili tena wa mchezaji ,ina maana kama itatokea mchezaji anaumwa ndio basi tena na usiombe itokee kwa golikipa.

Napenda kukumbusha katika soka kwenye sheria no 3 (Players) inampa mamlaka makubwa kipa, Ni Mchezaji wa tofauti sana na wale wenzake wa ndani,ndio maana katika sheria hii ,inasema watacheza wachezaji 11 kwa pamoja na wakipungua wawe 7 lakini lazima kipa awepo.

Wangapi wanakumbuka Mechi iliyomfanya Golikipa wa Chelsea /Arsenal Peter Cech avae kofia pale anapocheza Soka hadi Leo? katika mechi ile kipa Wa Pili Wa Chelsea pia aliumia Carlo Cudicin na beki john Terry akalazimika kurudi Golini ,sasa utofauti hapa upo sehemu moja kwamba katika usajili Wa wachezaji 23 ukitoa wachezaji 11 wanaoanza wale kumi na 12 wote wanakuwa mchezoni ina maana makipa wawili wanakaa nje na likitokea lolote la kutokoea wanaweza kucheza wote watatu katika game moja

Bado na’connect’ na sababu yake ya kwenda na makipa 5 kutokana na umuhimu wa nafasi hii na hasa inapokuja suala la mechi mbili za kirafiki kabla ya Siku ya mwisho ya usajili, akilini mwake Kocha anajua nani ni kipa wake No 1 nani 2 nani 3 wawili wengine ni kama tahadhali tu endapo kutatokea majeruhi.

Imeandaliwa na Tigana Lukinja, mchambuzi na mwalimu wa mpira wa miguu.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x