Sambaza....

Leo kuna mechi ambayo inawakutanisha Liverpool na Manchester City katika uwanja wa Anfield.

Mechi ya mzunguko wa kwanza Manchester City alifanikiwa kuifunga Liverpool goli 5-0.

Leo hii wanakutana wakati ambao Liverpool anatafuta nafasi ya kubaki kwenye nafasi nne za juu na Manchester City akitafuta nafasi ya kujichimbia juu.

Manchester City mpaka sasa hajafungwa na katika michezo yote aliyocheza msimu huu ni mchezo mmoja tu ambao kamaliza bila kufunga goli ( dhidi ya Crystal Palace).

Leo anaenda kwenye uwanja wa Anfield, nafasi yake ikoje? Ana nafasi ya kupoteza mechi hii?

Manchester City ana nafasi ngumu katika uwanja wa Anfield leo hii kutokana na sababu zifuatazo.

Liverpool wanaingia bila Philippe Countinho kwa mara ya kwanza. kuna uwezekano mkubwa timu zote zikaingia na mfumo wa 4-3-3.

Mfumo huu utakuwa na manufaa kwa Liverpool kwa sababu kwa siku hivi karibuni Liverpool wamekuwa wakitumia vizuri mipira ya krosi wanazopiga na Manchester City kwa siku za hivi karibuni wamekuwa wakishindwa kujilinda vizuri pindi mipira ya krosi inapokuja langoni mwao.

Mfano katika mechi dhidi ya Huddersfield town, Otamendi alijifunga kutokana na krosi iliyopigwa langoni mwao, Westham United walifunga goli pia kutokana na krosi. Mifano hii inaonesha dhahiri Manchester City hawajui kukaba vizuri pindi krosi zinapokuja kwao.

Ushindi mwembamba wa mechi za hivi karibuni inaonesha timu nyingi zimeshajua kucheza na Manchester City ?

Kadri muda unavyozidi kwenda kasi ya Manchester City katika viwanja vya ugenini imeanza kupungua.

Mwezi wa kumi na mbili, wamefungwa na Shakhtar Donetsk katika michuano ya UEFA ikiwa ndiyo mchezo pekee ambao msimu huu wamepoteza.

Wakaja kushinda ushindi mwembamba dhidi ya Newcastle United katika uwanja wa St. James Park, pia wakaja kutoa suluhu na Crystal Palace katika uwanja wa nyumbani wa Crystal Palace.

Hii inaonesha kasi yao inapungua pale wanapocheza katika viwanja vya ugenini.

Hali ya hewa ya uwanja wa Anfield itakuwa na nguvu kwa Liverpool?

Bila shaka Liverpool wanafaida kubwa ya kucheza katika uwanja wa nyumbani. Uwanja ambao una mashabiki walevi wa soka wanaosimama na wachezaji mwanzo hadi mwisho wa mchezo, hii itakuwa faida kubwa kwa liverpool kwa sababu wachezaji wake watatiwa nguvu kubwa kutoka kwa mashabiki.

Rekodi ya mbaya ya Manchester City pale Anfield ina nguvu kubwa kwenye hii mechi ???

Manchester City hawajawahi kushinda katika uwanja wa Anfield kwa miaka 15 mfululizo. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2003.

Rekodi hii inaweza ikaathiri pande zote mbili kutokana na jinsi gani kila upande itakavyochukulia.

Mfano, kama Manchester City wataichukulia kwa hofu rekodi hii basi watakuwa na nafasi kubwa ya kucheza kwa hofu, na unapocheza kwa hofu unapata nafasi kubwa ya kufanya makosa mengi binafsi ambayo yanampa nafasi adui kukuadhibu.

Ila kama wakiichukulia rekodi hii kawaida watacheza kwa utulivu zaidi, tofaufi na kama ambavyo watakavyopania kuivunja rekodi hii kwa sababu watajikuta wanafanya makosa mengi binafsi kutokana na kutokuwa makini.

Liverpool rekodi hii inawapa nafasi kubwa ya kuingia bila hofu hali ambayo itawafanya wajiamini, ila wakijiamini kupitiliza kutakuwa na madhara makubwa kwao tofauti na kama wakijiamini kiasi.

Rekodi ya Jurgen Klopp dhidi ya Pep ina nafasi gani katika mchezo wa leo ??

Hakuna kocha mwenye rekodi nzuri dhidi ya Pep Guardiola kama Jurgen Klopp.

Wamekutana katika michezo 11, wote wameshinda michezo mitano na kutoka sare mchezo mmoja kila mmoja.

Takwimu hizi zinaonesha Jurgen Klopp siyo mnyonge kwa Pep Guardiola hali ambayo inamuongezea sababu ya yeye kushinda mechi ya leo.

Mashambulizi ya kushitukiza yana nafasi kubwa ya kuimaliza Manchester City?

Hapana shaka ndipo ilipo siri ya kuifunga Manchester City ambayo muda mwingi hutamani kwenda mbele, hivo kuwatumia wachezaji wenye kasi kama Saido Mane, Mohamed Salah kutakuwa na nafasi kubwa ya Liverpool kuwa na nafasi ya kuwafunga Manchester City kupitia mashambulizi ya kushitukiza.

Urejeo wa Mohamed Salah utakuwa na faida kubwa kwa Liverpool?

Hapana shaka,msimu huu akiwa na goli 22 kwenye mashindano yote na goli 17 kwenye ligi kuu ya England.

Ni mhimili mkubwa sana kwenye safu ya ushambuliaji ya Liverpool.Hivo kurejea kwake kutakuwa kumeipa nguvu zaidi ƘLiverpool.

Uwepo wa Van Djik una nafasi gani kwenye eneo la ulinzi kwa Liverpool?

Mechi ya mwisho Liverpool alifungwa goli 5-0. Liverpool ambayo ilikuwa na matatizo ya ulinzi.

Tofauti na muda huu wanapokutana ambapo Liverpool kwenye sehemu yake ya ulinzi kuna mabadiriko.

Gomez kwa sasa kaimarika tofauti na mwanzo ambapo timu hizi zilivyokuwa zinakutana.

Amecheza kwa miezi 6 anaonekana kuimarika siku baada ya siku, Van Djik ni beki bora na anakuja kuondoa makosa binafsi ambayo yalikuwa yanafanywa kipindi cha nyuma na mabeki wa kati wa Liverpool.

Kupumzika siku tisa kwa Liverpool itakuwa na faida?

Manchester City wamecheza katikati ya wiki na kufanya mabadiriko machache kwenye kikosi ila wachezaji wake muhimu kama Fernandhinho, David Silva, Raheem Sterling, Sergio Aguero walianza.

Wakati huo Liverpool wakiwa Dubai, hii inawapa nafasi kubwa Liverpool ya kutokuwa na uchovu tofauti na Manchester City.

Sambaza....