Luc Eymael, Kocha wa Yanga sc
Blog

Luc Eymael ampiga mkwara Mkwasa, amrudisha Molinga

Sambaza....

Juzi Kulikuwa na hali ya sintofahamu kati ya mshambuliaji wa Yanga SC , David Molinga “Falcao” na kocha msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa . David Molinga alitolewa kwenye timu na kocha huyo msaidizi.

Charles Boniface Mkwasa alimtoa David Molinga kwenye kikosi cha Yanga kutokana na David Molinga kuzidi uzito kwa kilo 12 pamoja na kukosa “fitness” kitu ambacho kilimpelekea Charles Boniface Mkwasa kumsimamisha David Molinga .

David Molinga “Falcao”

Baada ya David Molinga kusimamishwa na Charles Boniface Mkwasa, David Molinga alidai kuwa kocha huyo msaidizi hampendi David Molinga tangu zamani na kisa cha kumsimamisha ni chuki kwa sababu David Molinga alidai kuwa hajaongezeka kilo 12 kama ambavyo kocha huyo alisema ila yeye kaongezeka kilo 3.

Kipindi ambacho haya yanafanyika kocha mkuu wa Yanga , Luc Eymael alikuwa nje ya nchi . Baada ya yeye kusikia sakata hili la David Molinga pamoja na Charles Boniface Mkwasa aliamua kumrudisha kwenye kikosi cha Yanga mshambuliaji huyo kutoka Congo . Kurudishwa kwa mshambuliaji huyo kunaonesha namna ambavyo Charles Mkwasa alivyokuwa na sauti ndogo kwenye kikosi cha Yanga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.