EPL

Man U yapigwa viwili vya haraka haraka

Sambaza....

Ushindi wa kwanza wa Nigel Pearson kama kocha mkuu wa Watford umepatikana Leo ndani ya dakika 4 wakifanikiwa kufunga magoli 2 dhidi ya Manchester United.

Ismail Sarr alifunga goli la kwanza goli ambalo lilitokana na uzembe wa golikipa David De Gea,  Wanna – Bissaka alisababisha penati ambayo aliifunga nahodha wa Watford  Deeney.

Matokeo hayo yameibakiza Watford katika nafasi ya mwisho mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 12 ikiwa nyuma ya alama 7  na Southmpton inayoibuka nafasi ya 17, nafasi ambayo siyo hatari kushuka Daraja.

Manchester United katika mechi 18 wamefanikiwa kuchukua alama 25 , alama chache sana kuwahi kuzipata kwenye kampeni ya ligi kuu England.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.