Msemaji maarufu wa Simba Sc, Hadji Manara
Blog

Manara: Simba ni zaidi ya Gor Mahia, APR na Yanga.

Sambaza kwa marafiki....

Msemaji wa klabu ya Simba Hajji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ametamba kua klabu yake ya Simba ndio klabu ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kua “verified” katika mtandao wa Instagram.

Manara kupitia ukurasa wake ameandika “Klabu Bingwa nchini Tanzania imekua klabu ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kua Verified katika Account ya Instagram.
Yes Simba ndio klabu pekee ya michezo kupata verification hiyo (blue tick)
Ok wengine mtafwata huko dudu layuyu!”

Mpaka sasa ukurasa wa Simba una jumla ya wafuasi 585K (585,000) huku ukura huo wa Simba ukiwafuata watu 36 tu!

Kwa maana hiyo basi klabu ya Simba imevizidi vilabu vikubwa Africa Mashariki na kati kama Gor Mahia na Tusker (Kenya), APR na Rayon Sports (Rwanda), SC Villa na URA (Uganda) Yanga sc na Azam fc vya hapa nyumbani.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.