Ligi Kuu

Manula kuikosa Mbao FC

Sambaza kwa marafiki....

Golikipa wa Simba na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) ataikosa mechi dhidi ya Mbao Fc itakayochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Aishi Manula amekuwa na majeraha ya kidole ambayo yamemsababisha asifanye mazoezi kwa ukamilifu.

Pamoja na kwamba ameelekea Morogoro, lakini hatokuwepo kwenye sehemu ya mchezo huo kutokana na maumivu ya kidole yanayomkabili.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.