Blog

Mashabiki wa Yanga wamehamia kwa Kaseja na kumponda Manula-Magori

Sambaza kwa marafiki....

Kumekuwa na mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na Juma Kaseja pamoja na Aishi Manula kuwa nani anastahili kuwa Tanzania one .

Katika moja la group la michezo pameamkia mjadala huo mzito. Na ndani ya mjadala huo ndipo aliyekuwa mtendaji mkuu wa Simba bwana Magori alipoamua kutoa maoni yake kuhusu mjadala huu kama ifuatavyo;

Wapenzi wote wa Yanga wamehamia kwa Kaseja na kumponda Manula! Huu mpira jamani!

Nakumbuka wakati Yanga anafungwa na Simba bao 3-1 Mtani Jembe kwa moja ya goli lake la uzembe na hatimaye akaondoshwa Yanga, sijui akina Kaisi walikuwepo uwanjani! Mwenye clip aweke lile goli!

Mwaka 2003 Kaseja alikuwa nyota kuwatoa Zamalek pale Cairo! Mwaka huo huo tulifungwa na Enyimba kule kwao Aba goli 3-0! Goli zote zimepigwa mbali nje ya 18! Tukajiuliza ni huyu Kaseja tunayemjua? Huo ndio mpira! Tujifunze kwanza!

Kuna mengi mazuri tu amefanya Kaseja na kuna mapungufu mengi tu amefanya Kaseja pia! Hivyo hivyo kwa Manula!

Ila tunalo sahau, wakati Kaseja akielekea ukingoni, Manula bado ana miaka 10 na zaidi ya kudaka! Naomba atakapokuwa amefikia uzoefu wa aina ya Kaseja baada ya miaka 10 ndio tutaweza kutathmini nani kati yao alikuwa bora kwa statistics!”

Haya ndiyo maoni ya aliyekuwa mtendaji mkuu wa Simba, yapi maoni yako binafsi ?


Nani anafaa kuwa Tanzania One?

Loading ... Loading ...

 

Tafadhali tumia viungo rasmi kusambaza habari zetu. Facebook, Twitter au Barua Pepe. Kama utataka kutumia habari zetu tuandikie kupitia habari@kandanda.co.tz