Sambaza....

Kocha wa timu ya soka ya Mashujaa ya mkoani Kigoma Funga Machunga Amesema nidhamu ya mchezo ndio sababu ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mabingwa wa Tanzania Bara Simba SC katika mchezo wa raundi ya tatu michuano ya Azam Sports Federation Cup.

Manyundu amesema wachezaji wake walifuata maelekezo sahihi ambayo aliwaambia ikiwemo kutowaogopa wachezaji wa Simba licha ya kuwa na majina makubwa na uwezo mkubwa kuliko wao.

“Simba ni timu kubwa, tunawaheshimu, matokeo ya Jana yamechangiwa zaidi na nidhamu ya wachezaji, tuliwaambia wanacheza na timu kubwa hivyo lazima wacheze kwa nidhamu na kutumia ufundi zaidi kuliko nguvu,”

“Tulikuja na ari ya kushinda kwa maana tumetoka Burundi kwenye mashindano ya Ujirani mwema na kuchukua ubingwa kwa hiyo kwa hali hiyo tukajiuliza Kama tuliweza kule Basi na dhidi ya Simba tunaweza kuthubutu na kushinda,” amesema.

Kocha huyo ambaye alikuwa akiongea kwa bashasha amesema ushindi huo Unaendelea kuwajengea kujiamini kuelekea michezo ya Ligi Daraja la Kwanza Ili kutafuta nafasi ya kupanda Ligi kuu.

“Ujue ukitaka kupanda ligi ni muhimu kushinda dhidi ya timu hizi kubwa, na lengo letu ni kupanda Ligi kuu Ili hizi timu kubwa zije kucheza mkoani Kigoma, ushindi huu ni kama chachu ya kufikia malengo yetu,” amesema.

Sambaza....