Sambaza....

Aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu ya Simba Sc, ambaye hivi karibuni amekuwa akitajwa kuondoka katika klabu hiyo, Masoud Djuma sasa yametimia. Viongozi wa Simba pamoja na Masoud Djuma wamekaa kwa pamoja na kuvunja mkataba kwa makubaliano maalumu.

Taarifa ambazo tovuti ya Kandanda imepata zinasema Masoud Djuma, kocha huyo aliyejibeba umaarufu mkubwa huenda akatua katika klabu ya Yanga.

Tetesi zinasema leo atakuwepo uwanjani wakati Yanga itakapokutana na Mbao Fc. Habari hizi bado hazijathibitishwa, lakini punde tukipata habari kamili tutawaletea. Na inasemekana kocha mkuu wa Yanga , Mwinyi Zahera amempendekeza ili kuwa kocha msaidizi wake.

Ikumbukwe kuwa tangu aondoke Shadrack Nsajigwa , Yanga imekuwa haina kocha msaidizi.
Kitu muhimu cha kujiuliza, je anaenda kuwa mfalme au anaenda kuwa kama alivyokuwa Simba Sc? Fuatilia tovuti yetu kwa habari zaidi.

Sambaza....