Video

Mbwana Samatta, akitambulishwa kwa waandishi wa habari.

Sambaza....

Mbwana ‘Samagoal’ Samatta aakijibu maswali mbele ya mkutano na waandishi wa Habari, aliposajiliwa na klabu ya Genk ya Ubelgiji.

Samatta ameelezea kufurahishwa na kujiunga kwake katika klabu ya Genk, na yupo tayari kuisaidia timu hiyo kushinda mabao ambayo yataiwezesha klabu hiyo kupata mataji.

Anategemea kuwa na misimu mizuri hapo Genk, ili aache historia kama alivyoaacha TP Mazembe pia.

Ameelezea pia kwanini alichagua namba 77, alipendezwa avae 7 kama kina Cristiano Ronaldo, Cantona lakini ili kupunguza msuguano wa kugombea namba ndio maana akaomba 77. Hivyo yeye yawezekana ni zaidi ya hao, akiwa na double 7, 77.

Kila la Heri.

Chanzo: Video imetengenezwa kutokana na video iliyowekwa youtube na Klabu ya Genk

Sambaza....