Ligi

Molinga agoma na kususa tena YANGA

Sambaza....

Leo kwenye mechi ya ligi kuu Kati ya Yanga na Biashara United kwenye uwanja wa Taifa , kulitokea kitu kimoja ambacho kimebaki kuwastaabisha wengine.

Wakati kipindi cha pili kikianza tulishuhudia mshambuliaji mpya Yikpe Dominick akiingia uwanjani kuchukua nafasi ya David Molinga.

Lakini cha kushangaza Yikpe Dominick aliingia moja kwa moja uwanjani bila kufanyiwa mabadiliko kama inavyokuaga kutokana na David Molinga kususa.

David Molinga hakuwepo uwanjani na hata kipindi cha pili kuanza alionekana ana nguo za kawaida na siyo jezi za Yanga huku akiwa hayupo kwenye Benchi is ufundi la Yanga.

Hii siyo mara ya kwanza kwa David Molinga kuonekana kutofurahishwa na mabadiliko ambayo hufanyiwa na kocha Charles Boniface Mkwasa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.