Benard Morrison
Blog

Morrison akamatwa na Polisi

Sambaza....

Mshambuliaji wa Yanga leo amekamatwa na jeshi la polisi baada ya kukutwa na kosa ambalo lilisababisha akamatwe. Taarifa hii imedhibitishwa na kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi na kamanda wa polisi Kinondoni.

Kamishna msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi na kamanda wa polisi Kinondoni Rodgers Bukombe amesema “Morrison alikamatwa leo mchana baada ya kupishana maneno na vijana wetu ambao walikuwa wanatilia shaka gari lake baaada ya kumsimamisha kulikuwa na ukaidi fulani”

Askari anapokuwa doria anapotilia shaka kitu chochote huwa anataka ajiridhishe na uhalali juu ya kile kilichopo kwenye eneo hilo. Walitaka kujua kwenye gari lake kuna nini kukatokea mabishano”- alisema kamanda huyo wa polisi kanda ya Kinondoni.

“Lakini yeye mwenyewe aliomba wampeleke polisi na kweli vijana walimchukua na baaada ya kumfikisha maelezo yaliyotolewa ikaonekana kwamba ni kosa la kawaida ambalo siyo lazima aendelee kushikiliwa kwa hiyo akawa ameachiwa kwa dhamana” alimalizia kamanda huyo wa polisi Kindondoni


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.