Ligi Kuu

Mpole ni sugu aliahidi ufungaji bora!

Sambaza....

Baada ya George Mpole kufanikiwa kuibuka kinara wa mabao katika Ligi Kuu ya NBC  “Mpwa” Tigana Lukinja ametoa ya moyoni kuhusu kinara huyo wa mabao aliefanikisha kuibakiza tuzo hiyo nyumbani na kumpiku Fiston Mayele.

“Alistahili kabisa wakati wenzake wako na magoli 10 lusajo na Mayele yeye alikuwa na 6 akaniambia atakuwa mfungaji bora, nikamtia moyo anaweza maana nimepata kumfundisha tukiwa lipuli 2015/16 ligi daraja la kwanza dogo (Mpole) ni sugu na jasiri sana hana uwoga hata kidogo na ni mtu wa kujitoa mhanga na ni mpambanaji haswa.”

George Mpole.

Mpole ambae pia ni mshambuliaji wa Timu ya Taifa amefanikiwa kufunga mabao 17 na kumzidi Fiston Mayele (16) wa Yanga.

George Mpole ambae amepita vilabu mbalimbali kama Majimaji Fc, Polisi Tanzania na Mbeya City ni mara yake ya kwanza kuvuka magoli matano katika Ligi Kuu toka alipopita katika vilabu vyote hivyo.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.