Ligi Kuu

Mshambuliaji wa Yanga aifuata rekodi ya Kagere na Chirwa!

Sambaza....

Nyota wa zamani wa klabu ya Ndanda fc Atupele Green amefanikiwa kufunga mabao matatu yaani Hatrick katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya klabu yake ya Biashara United dhidi ya KMC.

Atupele amefunga mabao hayo jana na kuiwezesha klabu yake kushinda mabao manne kwa sifuri  mbele ya KMC katika uwanja wa Karume Musoma na kujihakikishia alama tatu kwa Wanajeshi hao wa mpakani.

Atupele Greeb akithibitiwa na Paul Ngalema

Atupele Green mchezaji wa zamani wa Yanga sc na Ndanda kwa kufunga mabao hayo anakua mchezaji wa sita msimu huu kuweza kufunga mabao matatu katika mechi moja.

Wachezaji wengine walifunga hatrick msimu huu ni pamoja na Meddie Kagere (Simba sc), Obrey Chirwa (Azam fc), David Ulomi (Alliance School), Daruesh Saliboko (Lipuli fc) na Kevin Kongwe Sabato (Kagera Sugar).

 

Sambaza....