Ligi Kuu

Msuva: magoli saba yanatosha kabisa.

Sambaza....

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga ambae kwasasa anaitumikia KMC “Kino Boys”  James  Happygod Msuva amesema wanapambana kimwili na kiroho timu isishuke daraja endapo Ligi itarudi kuchezwa tena.

James Msuva amezungumzia malengo yake  binafsi kama mchezaji lakini malengo ya timu kwa ujumla baada ya Ligi kurudi ili kumalizia michezo 10 iliyobaki pindi ambapo hali itakua shwari na serikali kuruhusu michezo kuendelea kama kawaida.

James Happygod Msuva.

Msuva “Kama wachezaji kila mtu ana malengo yake, lakini ukiyakusanya yote unapata malengo chanya kwaajili ya timu ambayo yatasaidia timu ili ligi ikiisha tuwe katika nafasi nzuri.

Tunashukuru muunganiko ulikua mzuri (kabla ya Ligi kusimama), umoja na mshikamano ulizidi pia. Malengo yetu ni kubaki ligi kuu ndomana uliona tulicheza vile, hatutaki timu ishuke daraja.

James pia hakusita kuzungumzia malengo yake binafsi haswa katika ufungaji mabao ambapo mara nyingi amekua akikatishwa kasi yake kutokana na majeraha ambayo amekua akiyapata mara kwa mara.

James Msuva baada ya kupata majeraha katika mchezo dhidi ya AS Kigali.

“Malengo yangu Ligi ikirudi kwa mechi hizo zilizobaki ni kufunga magoli 7, naamini nitafanikiwa. Kwa mawazo, nguvu niliyonayo mimi na wenzangu naamini tutafanikiwa.” James Msuva.

Kabla ya Ligi Kusimama KMC ilikua imepata ushindi katika michezo minne mfululizo na kufanya kusogea mpaka nafasi ya 15 katika msimamo.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.