Ligi Kuu

Mtibwa kujenga uwanja wa kisasa.

Sambaza kwa marafiki....

Baada ya taarifa kutoka kwenye bodi ya ligi kuu Tanzania bara kuvifungia viwanja vitatu vya Manungu ambao unatumiwa na klabu ya Mtibwa Sugar, Mabatini unaotumiwa na Ruvu Shooting pamoja na Mwadui Complex unaotumiwa na Mwadui FC.

Mtandao huu ulimtafuta afisa habari wa klabu ya Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru. Kifaru amedai taarifa imekuja imechelewa sana

“Wameleta taarifa muda ukiwa umeenda sana, walitakiwa kutoa taarifa mapema kuliko kuleta taarifa muda ukiwa umeenda”.

Alipoulizwa kuhusu uwanja gani watautumia kama Mtibwa Sugar, amedai kuwa hawatoenda nje ya mkoa wa Morogoro.

“Tutatumia uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, hatuwezi kuhama nje ya mkoa wa Morogoro kwa sababu hii ni klabu ya Morogoro”- alidai msemaji huyo wa Mtibwa Sugar.

Alipoulizwa kuhusu madhara hasi watakayopata kuhusu kutumia uwanja wa Jamhuri amedai kuna madhara hasi sana.

“Kwanza tutakuwa tunatumia gharama kubwa, kwa sasa tunaweza kutumia zaidi ya milioni nne kwa ajili ya kusafirisha timu kutoka Manungu mpaka Morogoro, kukodi hotel kwa ajili ya wachezaji wetu, kwa hiyo kutakuwa na madhara hasi makubwa kwetu sisi “.

Alipoulizwa kuhusu kutafuta suluhisho la muda mrefu, amedai kuwa Mtibwa Sugar wana mpango wa kujenga uwanja wa kisasa.

“Sisi tunaendelea na utaratibu wa kujenga uwanja mkubwa wa kisasa, tumeshapata eneo la kujenga uwanja, na tuko kwenye taratibu za kuanza ujenzi rasmi”- alidai Afisa Habari huyo wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.