Blog

Mtibwa Sugar, ZFA wametoa neno sakata lá kufungiwa kwa kiungo wa Yanga!

Sambaza....

*Chama cha soka chá visiwani  Zanzbar ZFA nao wametoa maoni yao kuhusu sakata lá kufungiwa kwa mchezaji Mohamed Issa “Mo Banka”, huku wakijitoa na kuiachia mzigo TFF.

ZFA wamenena hivi “Ripoti ya vipimo vya Mo Banka zipo TFF hiyo ni siri sisi hatujui wenye kujua ni TFF maana hao ndio wanachama wa FIFA”.

Kwa Upande wa Mtibwa Sugar:

Nae msemaji wa Klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro wametoa ya moyoni kuhusu sakata hilo huku wakiweka wazi kua hawakutaka mchezaji huyo atue Yanga kwani baro walikua wanamuhitaji kiungo huyo.

Thobias Kifaru amesema “Mohammed Issa “Banka” sisi tulimlea kijana alipata uwezo mkubwa hapahapa Mtibwa baada ya mkataba wake kuisha tulimwomba aongeze mkataba akakataa tukamwambia sawa nenda hiki ni chuo kikuu bwana wamepita wengi nenda ukimaliza mzunguko utarejea kuhusu taarifa zake sisi hatujui waulizeni klabu yake Yanga ndio wanajua alipo”

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x