Sambaza....

Uchaguzi wa Simba umemaliza Jana usiku wa saa nane ambao ndiyo muda ambao wa matokeo yalipotangazwa. Uchaguzi huo umeshuhudia baadhi ya viongozi ambao walikuwepo katika awamu iliyopita kutochaguliwa tena.

Viongozi ambo walikuwepo katika awamu iliyopita na hawakuweza kufanikiwa kutetea nafasi zao ni wajumbe wa kamati tendaji ambao ni Iddy Kajuna, Said Tully, Ally Suru na Jasmin Soud.

Mwina Kaduguda akiteta jambo na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Simba, Try Again.

Katika Uchaguzi huo , tumeshuhudia Swedi Khamis Mkwabi ndiye mwenyekiti mpya Simba SC. Na tukashuhudia wakichaguliwa wajumbe wa kamati tendaji ya Simba ambao wataingia moja kwa moja kwenye bodi ya Simba kama Wajumbe wa bodi ya wakurugenzi Simba SC ni Hussein Kitta Mlinga, Selemani Harub Said, Dr. Zawadi Ally Kadunda, Asha Ramadhani Baraka na Mwina Kaduguda.

Yafuatayo ni matokeo ya Jumla ya Uchaguzi huo.

Mwenyekiti


Sued Mkwabi kura 1579 kati ya 1628

WAJUMBE:


Asha Baraka. -1180
Hussein Kitta. – 958
Dr Zawadi. – 830
Seleman Harub. -740
Mwina Kaduguda -577
Elia Alfred Martin. -530
Juma Pinto. – 440
Jasmin Soud. – 368
Patrick Rweyemam-349
Abubakar Zebo. -301
Iddi Kajuna. -270
Said Tully. -247
Ally Suru. -217
Chris Mwansasu -186
Hamis Mkoma. -174
Mohamed Wandwi-124
Abdallah Migomba -97

Sambaza....