Makambo akiwa katika klabu ya Horoya
Ligi Kuu

Mwinyi Zahera ni meneja wa Makambo ?

Sambaza kwa marafiki....

Hapana shaka kawa na msimu mzuri sana chini ya Yanga. Hili halina ubishi kabisa na ni jambo ambalo linaonekana kwa macho ya nyama.

Ndiyo timu pekee ambayo mpaka sasa hivi inampa changamoto Simba katika mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara.

Simba hii ambayo ni bora, Simba hii ambayo inaogopeka kwa sasa. Simba hii yenye huduma nyingi nzuri kuzidi timu yeyote kwa sasa hapa Tanzania.

Huduma wanayopata Simba huwezi kuifananisha na huduma inayopata timu nyingine ikiwemo Yanga.

Lakini Yanga bado inampa changamoto kubwa sana Simba mpaka sasa pamoja na kwamba timu yao haina huduma bora.

Hiki ni kitu kikubwa sana na ni kitu ambacho kocha wa Yanga , Mwinyi Zahera anastahili pongezi sana katika hili.

Kuwafanya wachezaji waweze kupigana katika mazingira magumu mpaka kufikia hatua kubwa sana kwenye ligi kuu.

Zahera

Kitu hiki kimemjengea heshima kubwa sana Mwinyi Zahera kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga mpaka sasa hivi.

Kuanzia viongozi, mashabiki na wanachama wa Yanga wote wanamweheshimu sana Mwinyi Zahera kwa sababu tu wamefanikiwa kuwa kwenye ushindani licha ya hali mbaya ya uchumi kwenye timu.

Kuna ile hali ya uoga ambayo inaonenaka kwa viongozi wa Yanga. Wanamuogopa sana Mwinyi Zahera kwenye kila kitu anachokifanya.

Kuna wakati Mwinyi Zahera hujivisha majukumu ambayo hayapo ndani ya mikono yake lakini viongozi hunyamaza na kumtazama tu.

Hakuna anayemkemea kwa sababu tu ya uoga walionao kwake na hii ni kutokana na Mwinyi Zahera kuiwezesha Yanga kufanya vizuri ingawa haiko katika mazingira mazuri kiuchumi.

 

Jana kulikuwa na habari ya Makambo kusajiliwa na klabu moja ya nchini Guinea. Lakini cha kushangaza hakuna kiongozi yeyote aliyeenda na Makambo kule Guinea.

Mtu pekee ambaye alienda na Makambo kule Guinea ni kocha huyo wa Yanga, Mwinyi Zahera. Hapo ndipo unaweza kujiuliza maswali mengi sana.

Mwinyi Zahera anaenda na Makambo kama nani ? Msimamizi wake yani Meneja wake ? Au anaenda na Makambo kama kiongozi wa Yanga?

Yani mchezaji wa Yanga ambaye ana mkataba na Yanga asajiliwe na klabu nyingine afu kwenye kusaini mkataba kusiwepo na kiongozi wa Yanga?

Hapa ndipo panapoonesha udhaifu wa viongozi wa Yanga mbele ya Mwinyi Zahera. Kisa tu Mwinyi Zahera kawasaidia katika nyakati hizi ngumu wanazopitia.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.