Nyoni akitetema baada ya kufunga penati katika mchezo dhidi ya Uganda iliyopelekea Tanzania kufuzu Afcon nchini Misri.
Blog

Mzizi wa Mafanikio ya Stars ni Azam Fc.

Sambaza....

KHuu ushindi wa Stars ni chimbuko la Wachezaji wa Azam Fc. Nimegundua kuwa mafanikio ya soka yanahitaji uwekezaji mkubwa sana. Bila ubishi njia pekee ya kuweza kupata mafanikio hayo katika timu ya taifa ni Either uwekeze katika kuwatoa wachezaji wengi nje ya nchi au ujenge misingi Bora ya Academy ambayo inawafungamanisha wachezaji wengi wa Timu ya taifa..na uwekezaji wenu umekuja kujibu katika national team.

Manula

Katika kikosi Kilichoitwa Stars Kuna lundo la wachezaji waliowahi kucheza Azam kama ni vijana au Timu kubwa au wanacheza Azam kwa Sasa.
Achana na Wafungaji katika mchezo wa jana ila hebu tathmini hiki kikosi


1.Aishi Manula
2.Erasto Nyoni
3.Gardiel michael
4.Aggrey Moris
5.Mudathir Yahya
6.Farid Mussa
7.Shaban Chilunda
8.Rashid Mandawa
9.John Bocco
10.Simon msuva
11.Yahya Zaidi
12.Himid Mao
13.Metacha Mnata


Athari ya Mawasiliano na Muunganiko Mzuri katika Academy Bora yamepelekea Matunda Bora katika Taifa letu.

Mabati ya Azam Fc, Yamenawirisha paa la Simba

Nahisi hayatasemwa, hayataandikwa lakini Ndio Grassroot ya mpira wetu na AzamFC wanastahili pongezi na Inapaswa Tff waendelee na Falsafa Ambayo Azam Wameicement.

Hongereni na Azam FC

Imeandaliwa na mdau wa Kandanda, Alex Nchimbi.-

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x