Sambaza....

Tovuti ya kandanda inahifadhi kumbukumbu za idadi ya magoli yaliyofungwa wakati wa mechi za Ligi Kuu, Tukiwa na lengo la kuwazawadia wachezaji wanaoongoza katika ufungwaji magoli kila mwezi. Kwa mwezi uliopita (Wa nane), Meddie Kagere ndio alikuwa kinara wa mabao.

Mwezi utafungwa kwa mechi kali ya watani wa jadi, Simba vs Young Africans SC ,baada ya hapo tutakuwa tumepata nani kinara wa mabao kwa mwezi wa tisa.

Meddie Kagere kama atacheza mechi dhidi ya Yanga, na kufunga, itamuongezea nafasi ya kuwa galacha wetu wa mabao mwezi huu kama wengine watashidwa kuziona nyavu.

Lakini sio Kagere tu, Stamili Mohamed Mbonde alifunga jana dhidi ya Mwadui, na kufikisha mabao 4, David Ambokile Eliud pia ameshafikisha mabao manne mpaka sasa.

Tano bora ya Wafungaji Mabao

Wapo wachezaji wengine wengi wenye magoli matatu, ambao kama watafanikiwa kufunga mabao ya kutosha, inaweza kuwashusha hawa tuliowataja. Habibu Kyombo, Hakizimana Kitenge, Bigirimana BlaiseVitalis Mayanga na Tafadzwa Kutinyu wanafukizia nafasi hii kwa kasi zaidi.

Je nani unadhani ataibuka galacha wa mabao mwezi huu, kuwa wa kwanza kutupa utabiri wako katika eneo la maoni ujishindie fulana ya GALACHA kutoka Kandanda.co.tz.

Sambaza....