Viongozi wa Yanga na GSM katika hafla ya utiaji saini ya uhusiano na Laligaga
Blog

Nifukuzeni Yanga – Mwakalebela

Sambaza....

Makamu mwenyekiti wa Yanga , Fredrick Mwakalebela amedai kuwa amechoshwa na maneno mengi yanayotokea ndani ya klabu hiyo, maneno ambayo yanarushwa kwake kila uchwao. Hali ambayo imemchosha mpaka kufikia hatua ya kulia.

Akiongea na kituo cha WASAFI FM huku akilia , Fredrick Mwakalebela amedai kuwa ameanza kuandamwa tangu zamani ila amekuwa kimya ili kuleta utulivu ndani ya klabu ya Yanga.

Vikosi vya Simba na Yanga vikiingia uwanjani!

“Kwa kweli leo nimesikitika sana na ninaongea haya nikiwa natoa machozi , Mimi nimekuwa nikisemwa mambo mengi kuhusiana na Yanga lakini nimekuwa nikikaa kimya ili kuleta utulivu”. Amesema Fredrick Mwakalebela.

Akizungumza suala la yeye kudaiwa kuihujumu Yanga kupitia hotel ambayo imepangwa kwa Yanga kufikia kwenye mchezo dhidi ya Lipuli FC , Mwakalebela amedai kuwa yeye hajui chochote .

“Mimi nilikuwa nyumbani Iringa kumuuguza mama yangu hill kilole kwenye kituo cha Amani Centre , kituo cha kulelea watoto yatima.

“Nimefika juzi, jana na leo niko hapa Iringa , baada ya kufika hapa naambiwa nimebook hotel kwa ajili ya kuihujumu Yanga , jamani hiyo hotel wamebook watu wa ofisini na mimi sijui kitu”.

Fredrick Mwakalebela alimalizia kwa kilio huku akidai kuwa kama wamemchoka au kuchokana ndani ya klabu ya Yanga basi wamuache au waachane kabisa.

“Kiukweli naomba niseme kama kweli mmenichoka naomba niwaachie timu yenu , kama kweli tumechokana naomba niwaachie Yanga maana mimi nimechoka kila baya linalotokea Yanga ni la Mwakalebela” alimalizia Fredrick Mwakalebela huku akitoa kilio.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.