Blog

Njooni nyote tulisaidie Taifa

Sambaza....

“MUSAEADAT ‘UMA”

Binadamu wote wanahitaji msaada katika maisha yao, hasa mwanzoni na mwishoni. Hivyo ni muhimu kujenga tabia ya kuwa tayari kuutoa na kuupokea vilevile. Haya ni maneno niliyokuwa nikipewa kila siku na Mwalimu wangu Hayati Bulicheka Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amen!

Wakati naendelea kutafakari juu ya Maneno ya Maalim wangu Almaruhum Bulicheka nikakumbuka Taifa hili letu linavyohitaji Msaada, hakika Taifa linapaswa kusaidiwa na Muda wa kulisaidia Taifa hili ni sasa na si wakati mwingine, nimeitafakari timu yetu ya Taifa iilivyo hovyo, nikatafakari wawakilishi wa Taifa hili kwenye mashindano ya Vilabu kwa miaka 8 iliyopita jinsi walivyokuwa wakifungwa Kikondoo na vitimu vya hovyo jovyo tu na hapa ndipo nilipoona Hakuna namna yoyote ile Ni kuusaidia Umma huu wa Watanzania wanaopenda Soka hapa Nchini!

Fikiria timu inapangwa Kundi moja na Akina Rayon Sport, Gor Mahia na USM Alger kundi halina hata kigogo kimoja halafu inashindwa kupata Alama za kuwavusha kwenda Hatua ya Robo fainali tena kwenye mashindano ya Hadhi ya chini kuliko yale ya Mabingwa Afrika wakiishia kuwa wa Mwisho mara zote wakiingia kwenye makundi wakishindwa hata kufikisha Alama 5 tu, Jamani acheni tulisaidie hili TAIFA, Acheni tuusaidie huu Umma!

Fikiria timu inapangiwa kucheza na Timu kutoka Swaziland/ eSwatini halafu wanabutuliwa na kutolewa huko Swaziland/ eSwatini Mnyama Simba Sponga kaingia na Kumbutua mtu 4-0 huko huko kwao, yaani Unapangiwa Timu kutoka Botswana ndio kale Ka nchi kanakosifika kwa kuwa na Wanaume wavivu halafu wanakuja kuwabutua kwenye Uwanja wenu wa Nyumbani kweli?? Inasikitisha sana! Uwanja wenu, Kila kitu Chenu halafu mnabutuliwa kizembe zembe tu Muda muafaka sasa acheni tulisaidie hili Taifa!

Jamani narudia tena Umma wa Watanzania unahitaji Msaada mkubwa kutoka kwetu Simba Sponga, Club ya Watu, Timu ambayo huwa siku zote ndio inaandika Historia za Soka la Nchi hii, mwaka 1974 Simba Sponga walikuwa timu ya kwanza na ya mwisho kucheza Nusu Fainali ya Timu Bingwa za Afrika, Mwaka 1993 Simba Sponga walicheza Fainali ya Kombe la CAF na sasa toka kuanzishwa Mfumo wa Makundi wa Mashindano ya Afrika Simba Sponga inaenda kuweka Rekodi Mpya kwa kuwa Timu ya kwanza kutoka Nchini kucheza hatua ya Robo Fainali kutokea kwenye Kundi lenye Wana Fainali wawili mmoja wa Champions League na Mwingine wa Confederations Cup! Yes leo Saa moja tunalitimiza hili bila Mikingamo yoyote ile!

Siku za nyuma huko nilipata kuandika MARUFUKU KUTUMIA AKILI KWENYE NCHII HII hakika maneno yangu hayakudondoka Bure, nimelithibitisha hili katika kuelekea kwenye mechi yetu vs AS Vita kuna Kocha wa timu moja kaamua kwa makusudi kabisa kuitelekeza timu yake kwa kusema anakwenda kwao Congo wiki nzima lakini cha ajabu timu ipo Ipogoro yeye yupo Dar ili ashuhudie MABALAA yetu cha Ajabu eti wanasema anataka kuwasaidia Mbinu wapinzani wetu ? yaani hata huelewi atawapa Msaada gani ikiwa yeye tumembutua ndani ya mwezi tu, tena kabla ya Mechi alikuja na nahau nyiiiingi lakini baada ya Mechi hadi kiswahili alisahau ?! Akawa anaongea yeye Kifaransa halafu ana Tafsiri yeye mwenyewe, Yaani mtu anaetaka kuwasaidia watufunge yeye mwenyewe alishashindwa huku Shati alilovaa likiwa zito mwilini mwake! ACHENI NYIE

Taifa hili linahitaji Msaada kwa sasa tena Msaada ambao Yamkini unaweza kubadilisha mambo mengi sana kuanzia kwenye Siasa, Elimu, Michezo na Burudani! Taifa hili ambalo watu wanaotumia AKILI hawapati Mafanikio, bali watu wajanja wajanja tu tena wakipandishwa bila kuelewa wanapandaje Harmorapa alianza, akaja Dr. Shika, akaja Konki Masta akapewa sana Airtime kwa vitu vya Kijinga leo tunae Bwana Piere Mlevi wa Taifa, huyu hadi anapandishwa Ndege kwenda nje ya Nchi kuliwakilisha Taifa sasa Tunawauliza Wakenya huyu mlimchukua huko kwenu kufanya nini? Hata wenyewe hawajui! Hivi tunakosea wapi Lakini!? vitu vya Kipuuzi ndio vinapewa Daraja la Juu kweli kweli, Yaani sio Vyombo vya Habari, Sio Mazungumzo ya kawaida ya Wananchi!

Nalisikitikia Taifa hili ambalo wasomi wake wanajitahidi ku twist Mijadala ili iwafanye wasionekane kupinga visivyokuwa sahihi wala kusapoti visivyokuwa sahihi pindi wanapokuwa nje, hakika ni MARUFUKU KUTUMIA AKILI kwenye hii Nchi, Yaani Kocha wa Timu yao anaacha Majukumu yake ya Msingi kwa Timu yake inayojiandaa na Mechi ya Ligi Kuu kwa Takribani siku saba akiaga anaenda kwenye Majukumu ya Timu ya Taifa lakini anageuka mpokea wageni eti Mkataba wake unamruhusu kuiacha Timu yake bila yeye kwa Mechi ya Ligi ili tu apokee Timu inayokuja kucheza na Wapinzani wao kwenye Ligi kwamba Wageni hao wanafundishwa na Boss wake kwenye Timu yao ya Taifa na Wasomi wetu wanashangilia kwa kusema Yule ni Mcongo na Wale ni Wacongo aisee naomba HADIDU REJEA hili Taifa limerogwa na aliyeliroga amekufa inahitajika Msaada kwa huu Umma! Kuwaondosha kwenye Fikra hizi za Kitumwa! Eti kwani kuna Shida kwa Mcongo yule kuacha Majukumu yake yanayofanya Alipwe Mshahara? Kuna mlevi ananiuliza kwani analipwa Mshahara yule? Nimemwambia sasa kama Halipwi anafanyake kazi? Maana Mkataba wa Kazi ni Ufanye kazi na Mwisho upokee Malipo ya kazi yako!

Anyway Ushawaza masuala ya Kiweledi yanavyozungumzwa na Wasomi wetu ikiwa jambo halina Maslahi kwao? Basi acha nikupe kituko kingine ambacho kinahitajika kupatiwa Msaada eti wanasema Yule Kocha anawasaidia wale jamaa waifunge Simba Sponga yaani hadi unacheka aisee sasa Huyo mtu yeye na Timu yake wamebutuliwa hapo Taifa leo anakuja kutoa Msaada gani? Waligoma kupanda Bus lao kwamba limerogwa, Waligoma kupita kwenye Tunnel kwamba imerogwa, Waligoma kuingia kwenye Vyumba vya Kubadilishia Nguo kwamba vimepuliziwa Dawa wakaongea Yote halafu mwisho wakapigwa na Terminator Meddie Kagere Ndugu zangu naomba TULISAIDIE HILI TAIFA na nipo Serious kwenye hili!

LEO saa moja kamili Jioni Simba SPONGA tutakuwa kwenye DHIMA ya kuanza kulipatia MSAADA hili TAIFA LETU ndio Msaada kwenye Nyanja ya Mpira wa Miguu, Mchezo huu Maridhawa kabisa Duniani kote na Kauli mbiu yetu ni ile ile TUNATAKA KULIKOMBOA TAIFA HILI KUTOKA KWENYE UNYONGE, Tupo kufanya Mapinduzi, Mapinduzi Makubwa ya Soka na niwaambie tu hakuna Mapinduzi bila Damu kumwagika, DAMU LAZIMA IMWAGIKE ili upate kujitoa kwenye UNYONGE, Sasa nyie Ndugu zetu kaeni Pembeni mshuhudie tutakachowafanya wale Dolphin kutoka Congo na Baada ya MSAADA HUU kwenye Soka naamini tutapata Watu wengine wakutoa Msaada kwenye Nyanja nyingine huko!

Nia tunayo, Uwezo tunao na Nguvu tunazo za kulitekeleza Jambo hili Kubwa sana la Kuusaidia huu Umma kama alivyopata Kunidokeza Ndugu yangu wa Kuitwa Mufti Sheikh Mkuu kutoka Viunga vya Peking Maalim Steven kwenye maneno yake machache sana Leo hii namnukuu ……”Waarabu hapo Oman wanasema “musaeadat ‘uma” Wak’ti wa kulisaidia Taifa!”

MUDA WA KULISAIDIA TAIFA HUU KWENYE MEDANI YA FOOTBALL

NJOONI WOTE TUANDIKE HISTORIA MPYA

#SIMBANGUVUMOJA

Mdidi the Writer!

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x