Sambaza....

Mchezaji wa klabu ya Simba, Ramadhani Kichuya, leo katika ukurasa wake wa Instagram alitoa nafasi ya kuulizwa maswali na kujibu 50 ya kwanza. Moja ya wauliza maswali hayo alikuwa ni Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, ambae alimuliza Kichuya kama hajisikii vibaya katika timu nzima ya Simba kuwa yeye ndio mtu mfupi zaidi na mwenye kichogo mwiba.

Kichuya katika hali ya utani, (Bila shaka kama ilivyokuwa kwa Tshabalala), alimjibu kuwa Tshabalala yeye anajiona mrefu wakati ufupi wake ndio ulisababisha Dante (Mchezaji wa Yanga) amkose katika kichwa alichokoswa wakati timu yao ilipokutana jumapili iliyopita.

Swali la Tshabalala:


official_mohamedhussein15Hivi uJisikii vibaya team nzima ya Simba Sc ww ndo Mtu Mfupi halafu una kichogo Mwiba @kichuya_

Jibu la Kichuya:


kichuya_@official_mohamedhussein15 mpuuz ww unajiona mrefu,sema kichwa cha dante ungekuwa mrefu ushapigwa ila alikukosa sababu ya ufupi wafupi oyeeeee??? (jokes)

Bado tamko la tukio la Dante na Tshabalala bado halijatolewa maelezo na shirikisho la Kandanda Tanzania.

 

View this post on Instagram

 

Nitajibu watu 50 wa kwanza niulize chochote ??

A post shared by Shiza Ramadhani kichuya (@kichuya_) on


Sambaza....