BlogEPL

Peter Crouch: Natamani Liverpool wawe mabingwa, ila…….!

Sambaza....

Mshambuliaji wa Burnley inayoshiriki ligi kuu England Peter Crouch amesema anatamani sana kuiona Liverpool ikinyakua ubingwa lakini pia anatamani kunyakuwa alama tatu muhimu kwenye mchezo wao wa ligi watakapokuwa ugenini wakicheza na Liverpool mwishoni mwa juma hili.

Crouch mwenye umri wa miaka 38 amesema mara zote amekuwa akifurahia anapocheza kwenye uwanja wa Anfield, kupambana na timu yake ya zamani ya Liverpool, hivyo kwa chochote ambacho kitatokea kwenye mchezo huo wa Jumapili kitakuwa sawa kwakwe.

“Napenda kurejea Liverpool” Crouch ameliambia jarida la The Burnley Express, “Nina marafiki wengi bado, watu wengi ninaowafahamu kule ni mashabiki wa Liverpool, hivyo ni vizuri kurudi nyumbani, napenda sana kama kipindi kile tumeshinda FA Cup na tukaingia kwenye fainali za UEFA, ilikuwa ni kumbukumbu nzuri kwangu,”.

Burnley ambayo ipo nafasi ya 16 wakiwa na alama 30, alama tano kutoka mstari hatari wa kushuka daraja, watahitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka katika mazingira mazuri wakati Liverpool wao ambao wapo kwenye mbio za Ubingwa, ushindi dhidi ya Burnley utawafanya kuongeza matumaini ya kupambana na Manchester City waliopo kileleni kwa alama moja.

“Nina marafiki wachache ambao ni wapenzi kindakindaki wa Liverpool, ambao hawatakuwa na furaha na mimi kama ikitokea nikawafunga, lakini sisi kama Burnley tunataka ushindi wa alama tatu, itakuwa nzuri sana kama nitapata kufunga goli na pia ningependa kuona Liverpool wakichukua ubingwa msimu huu,” Crouch amesema.

Crouch aliwahi kuichezea Liverpool kati ya mwaka 2005 hadi 2008 akicheza michezo 85 na kufunga mabao 22, mafanikio makubwa ni kuisaidia Liverpool kucheza fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan akichukua nafasi ya Javier Mascherano, fainali iliyopigwa jijini Athens Ugiriki ambapo walipoteza kwa mabao 2-1.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.