Sambaza....

Baada ya kuondoka kwa Mshambualiaji Cristiano Ronaldo katika klabu ya Soka ya Real Madrid na kujiunga na Juventus Kumekuwa na maswali mengi je ni nani atavaa Jezi namba 7 ndani ya kikosi hicho cha Los Blancos.

Japokuwa Juventus walitangaza Mapema kabisa kumsajili nyota huyo lakini Bado kocha Julen Lopetegui amekuwa kimya kumtangaza mrithi wa Jezi namba Saba ndani ya Real Madrid.

Kwa mujibu wa jalida la Mundo Deportivo la nchini Uhispania wamemtaja kinda Mariano Diaz Kama ndiye ambaye anatengenezwa na Real Madrid kama mrithi wa Jezi hiyo yenye heshima kubwa.

Cristiano Ronaldo sasa ni mchezaji wa Juventus

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, anarejea Santiago Bernabeu baada ya mwaka mmoja, ulioshuhudia akiondoka chini ya utawala wa meneja Zinedine Zidane, kufuatia kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Mariano anatarajiwa kutangazwa rasmi katika mkutano na waandishi wa habari Leo Ijumaa, na shughuli hiyo itafanywa na Rais wa klabu Florentino Perez.

Mshambuliaji huyo wa Jamuhuri ya Dominican, alikuzwa na kituo cha kulea na kuendeleza vipaji kwa vijana cha Real Madrid, na alitumika kama mchezaji wa akiba katika michezo minane mwaka 2017, kabla ya kutimkia Olympique Lyonnais, ambapo amecheza michezo 30 ya ligi daraja la kwanza nchini humo (Ligue 1) msimu uliopita, na kufunga mabao 18.

Mpaka sasa Jezi ambazo hazina wenyewe Kwenye kikosi cha Real Madrid ni pamoja na namba 7, 15, 16 na 23 hivyo Mariano Diaz atakuwa na nafasi ya kuchagua Jezi gani ambayo itampendeza.

Je wewe mfuatiliaji wa Kandanda.co.tz Unadhani nani anapaswa kupewa jezi hiyo?

Sambaza....