Mabingwa Ulaya

Sababu tatu kwanini Ronaldo anaweza kutolewa UEFA

Sambaza kwa marafiki....

Usiku wa Ulaya unarudi tena, usiku ambao hubeba hisia za watu wengi sana kwa sababu mabingwa hukutana.

Leo hii Massimiliano Allegri ana mtihani mkubwa sana mbele ya Diego Simione, kwa sababu mpaka sasa hivi Diego Simione ana faida ya goli 2-0. Juventus wamebakiza swali mojà tu la kujibu, watapindua matokeo ?

Zifuatazo ni sababu tatu zinaonesha ugumu wa Juventus kupindua matokeo.

ATLETICO MADRID WANAUWEZO WA KULINDA MWAKA MZIMA

Hii ndiyo kazi ambayo wanaweza kuifanya kwa ufasaha kabisa chini ya Diego Simione.

Hawa wamezaliwa kwa ajili ya kujilinda, wanauwezo mkubwa wa kujilinda, wanapenda kujilinda na hufurahia zaidi wanapokuwa na kazi ya kujilinda.

Kwao wao kazi ya kujilinda ni nyepesi zaidi kuliko kazi ya kufunga, na ndiyo kazi ambayo kwao wao hutabasamu kila wanapopewa. Hawa wanauwezo wa kujilinda hata ndani ya mwaka mzima.

Msimu huu wameruhusu magoli manane, na kwenye mechi za hivi karibuni wamepata cleansheets mfululizo katika mechi tano zilizopita.

Hapa ndipo ugumu wa kwanza wa Juventus kupindua matokeo unapokuja. Anakutana na timu ambayo kujilinda ndiyo kazi yao ya kwanza ya msingi kabla ya kazi zingine.

CRISTIANO RONALDO HAYUPO TENA KWENYE MIGUU YAKE

Hii ndiyo michuano yake, ndiyo michuano ambayo yeye ndiye mfungaji bora wa muda wote. Ndiyo michuano ambayo hufunga sana.

Ndiyo michuano ambayo miguu yake hufanya kazi ngumu kuliko michuano yoyote. Lakini kwa bahati mbaya msimu huu Cristiano Ronaldo hayupo katika miguu yake.

Ameshaondoka , kapumzika kwa msimu huu. Haitaki tena michuano hii, hafungi sana kwa misimu mingine nyuma.

Mpaka sasa ana goli moja tu katika mechi tano alizocheza msimu za ligi ya mabingwa barani ulaya. Kushuka kwa kiwango cha Cristiano Ronaldo katika michuano hii kunaweza kukaleta ugumu kwa Juventus kupindua matokeo.

DIEGO SIMIONE NI MBABE WA TIMU ZA ITALY

Kuna vitu viwili vya kutazama hapa. Historia inaniambia kuwa katika timu ambazo hufunga magoli 2-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza kwenye hatua hii ya mtoano, 81% ya timu hizo hufuzu kwenda hatua nyingine.

Diego Simeone

Hapa Atletico Madrid wana nafasi kubwa kwenye hili. Pili Diego Simione amekutana mara 7 na timu kutoka Italy na akafanikiwa kushinda mechi 5 na kutoka sare michezo miwili.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.