Mbwana Samatta akiwa Aston Villa
Tetesi

Samatta huyoo West Brom

Sambaza....

Mshambuliaji na nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” huenda akatimkia katika klabu nyingine ya EPL baada ya kuonekana kama ziada katika kikosi cha Aston Villa baada ya kuwasili kwa washambuliaji wapya katika timu.

Aston Villa imemsajili mshambuliaji Ollie Watkins kutoka Brendford lakini pia inatarajia kukamilisha uhamisho wa nyota wa zamani wa Chelsea Betrand Traore kutoka Olympic Lyon kwa ada ya £17milioni, pia kuna mshambualiaji mwingine Keinan Davies.

Mbwana Samatta akifunga goli mbele ya walinzi wa Bornamouth

Kwa idadi hiyo ya washambuliani ni wazi sasa nafasi ya Samatta ya kucheza itakua finyu huku pia kocha wake pamoja na Villa kwa ujumla wanamuona ni kama amefeli baada ya kucheza michezo 17 na kufunga mabao mawili tu.

Baada kuanza kwa kipigo cha mabao matatu kwa sifusi West Brom wanahitaji mshambuliaji wa kwenda kuongeza nguvu katika eneo la mbele huku wakiona Mbwana Samatta ndio chaguo sahihi kwao.

Mbwana Samatta

West Brom Albion wanamtaka nyota huyo wa Tanzania kwa mkopo lakini wakitakiwa kupambana na Fernebache ya Uturuki ambao pia wanahitaji saini ya nyota huyo wa zamani wa Simba na TP Mazembe.

Sambaza....