Sambaza....

Nahodha wa timu ya Taifa, Mbwana Samatta, amenukuliwa akisema kukosa penati ni jambo la kawaida kwa mchezaji, na kwake yeye ilibidi afanye jitihada ili kufuta makosa yake.

Samatta alikosa penati iliyopatikana katika dakika ya 21, baada ya Simon Msuva kudondoshwa eneo la hatari. Mpira wake uligonga mwamba na kurudi uwanjani.

Lakini haikuwachukua muda mrefu sana baada Samatta mwenyewe kufanya jitihada ya nguvu na kusababisha bao la kwanza lilofungwa na Msuva, kabla ya yeye mwenyewe tena kufunga bao la pili kipindi cha pili.

Sambaza....