Ligi Kuu

Shabani Idd atupia tatu Prisons ikilalaa Chamanzi!

Sambaza....

Klabu ya AzamFc imeendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu Bara baada ya kufanikiwa kuifunga Tanzania Prisons katika dimba la Chamanzi.

Azamfc wamefanikiwa kupata ushindi mnono wa mabao manne kwa moja dhidi ya Tanzânia Prisons na kuzidi kujiweka katika nafasi nzuri ya kupigania nafasi ya pili mbele ya YangaSc.

Magoli ya Azam fc yamewekwa kimiani na mshambuliaji wake kinda Shabani Idd Chilunda aliefunga magoli matatu na Frank Dumayo aliefunga bao moja.

Shabani Idd amefunga mabao hayo katika dakika za 02, 30 na 45, huku Frank Dumayo akifunga goli lake katika dakika ya 22 ya mchezo. Bao pekee la Tanzania Prisons likifungwa katika dakika ya 70 na Mohamed Rashidy.

Kwa ushindi huo inaifanya AzamFc ifikishe alama 55 huku wakiwa nafasi ya pili wakifuatiwa na Yanga wenye alama  48 na Tanzânia Prisons katika nafasi ya nne wakibaki na alama zao 45.

Baada ya kufunga magoli matatu leo Shabani Idd Chilunda anaungana na Emmanuel Okwi, Obrey Chirwa na Marcel Boniventure Kaheza waliofunga mabao matatu katika mchezo mmoja msimu huu.

 

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x