Blog

Simba imekuwa bingwa kwa sababu ya udhaifu wa Yanga

Sambaza....

Walianza vizuri sana. Mechi kumi na sita za mwanzo wakishinda mechi kumi na nne na kutoka sare michezo miwili.

Huu mwanzo ulikuwa mzuri mno. Na ni mwanzo ambao ulitià matumaini makubwa ndani ya timu ya klabu ya Yanga.

Waliona wanaweza kuchukua ubingwa. Waliona kabisa inawezekana kuona mafanikio kwenye njaa. Hiki ndicho walichokuwa wanakiona.

Na ndicho ambacho walikiweka katika mioyo yao. Sawa walikuwa na mazingira mabaya kiuchumi, lakini kushinda mechi kumi na nne ndani ya mechi kumi na sita kilikuwa ni kitu chenye faraja sana.

Hakufikiria kabisa mbio ambazo walikuwa wanashiriki zilikuwa zinamwihitaji Philbert Bayi na siyo Usain Bolt.

Waliwekeza katika kupata mbinu za Usain Bolt. Hawakufikiria kabisa namna ya kumpata Philibert Bayi awasaidie kupata mbinu sahihi.

Na hata mechi hizo kumi na sita walizocheza bila kufungwa walicheza katika uwanja wao wa nyumbani mechi zote.

Hapa ndipo swali gumu la wao kuchukua ubingwa lilipoanzia. Hapa ndipo ubora wao ulipokuwa na mashaka makubwa sana.

Ni lazima kuhoji kama walikuwa na uwezo wa wao kucheza katika viwanja vya ugenini katika kiwango kile kile ambacho wanatumia katika uwanja wa nyumbani.

Mtu imara hushinda popote pale, lakini hiki kitu kilikuwa tofauti kabisa kwa Yanga. Hawakuwa na uwezo wa kushinda katika baadhi ya mechi muhimu za ugenini.

Wakati ambao alitakiwa kushinda ugenini ndiyo wakati ambao alikuwa anapoteza alama ambazo zilikuwa muhimu katika mbio za ubingwa.

Pumzi ambayo walianza nayo mwanzo haikuwa sawa na pumzi ambayo walimaliza nayo kwenye ligi. Hapo ndipo unapokuja kupata udhaifu wao.

Hii ilikuwa tofauti kabisa na kwa wapinzani wao Simba. Wao walikuwa na uwezo mkubwa wa kupambana katika viwanja vyote.

PosTimuPWDLFAGDPts
1Simba SC38296377156293
2Yanga SC38275656272986

Haikuwa shida kwao kupata matokeo chanya kwenye viwanja Vingi vya ugenini tofauti na kwa Yanga.

Mfano mechi ambazo zilikuwa zinaonekana muhimu kwa Yanga katika viwanja vya ugenini, Yanga alipoteza.

Na Simba alipoenda kwenye viwanja hivo alifanikiwa kabisa kushinda na hapo ndipo uwazi wa ubora kati ya Simba na Yanga ulipokuwa unaonekana kwa kiasi kikubwa.

Wakati Simba alipoenda Iringa na kushinda dhidi ya Lipuli ndiyo wakati ambao Yanga alienda Iringa na kufungwa dhidi ya Lipuli.

Hata wakati ambao Simba alipoenda Mara na kushinda dhidi ya Biashara United ndiyo wakati ambao Yanga alipoteza alama tatu dhidi ya Biashara United pale Mara.

Hapo ndipo utofauti na ubora ulipokuwa unaanza kuonekana. Kwa kifupi Yanga ilikuwa dhaifu kuanzia ndani na nje ya uwanja.

Na Simba ilikuwa imara kuzidi Yanga kuanzia ndani na nje ya uwanja ndiyo maana waliweza kuhimili mbio za kina Philibert Bayi.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x