Shirikisho Afrika

Simba kama noma na iwe noma robo fainali ileeeee

Sambaza....

Wekundu wa msimbazi wana’ Lunyasi’ leo watakuwa ugenini kupeperusha bendera ya nchi kama ilivyo kawaida yao

Game ngumu dhidi ya mgeni mwenyeji Asec Mimosa kule Benin ,kwanini ni mgeni ni mwenyeji?

Mimosa watacheza nje ya Taifa lao la Ivory Coast kwa kile tulichoambiwa ni kusitishwa kwa matumizi ya viwanja vya ndani kupisha ukarabati wa maanndalizi ya AFCON ijayo

Kiufundi hii ni advantage ya moja kwa moja ya Simba kwenye mchezo husika kwa kuwa wote wawili watakuwa wanacheza ugenini ,hasa kwenye eneo la mashabiki ambao shughuli yao kubwa huwa ni’ kuanikiza ‘kuwapa ushujaa kama si ujasiri wapambanaji wao

Hata kama kwa ukaribu wa kijiografia ( zone) wanaweza kupata mashabiki wenyeji wa Benin na wale watakaotoka nyumbani Ivory lakini ukweli ni kuwa watatofautiana vilivyo kama wangecheza nyumbani kwao kwa asilia

Game hii kwa jicho langu imebeba dhamana ya Simba kwenye kufuzu ikiwemo kuongoza kundi kundi

Simba anaingia hapa akiwa kinara wa kundi kwa point 7 akiwa anafuatiwa kwa ukaribu na Mimosa point 6 huku Berkane pia akifuatia kabla ya kumuangalia kwa mbali Gendrrmarie mwenye alama 4

Endapo Simba atapata alama moja akawa na 8 atakuwa na 90% za kufuzu kabla ya kuuangalia mchezo wa mwisho wa hapa nyumbani na Gendermarie

Akipata pointi moja leo atamfanya Mimosa kuwa na alama 7 ambazo huwenda akamaliza nazo kwa kuwa huku mchezo wa mwisho ni away kwa berkane kwa mazoea ya michuano hii kila moja anashinda kwake

Kwa maana hiyo mpinzani moja wa Simba atakuwa ametoweka vita vitabaki na Berkane

Nidhamu kubwa ya Ufundi ,mbinu ustahimilivu na stamina inaweza kuwapa Simba alama hiyo moja kama si zote tatu ambazo ni muhimu sana

Benchi la ufundi likatulize kichwa likafanye uteuzi mzuri wa kikosi kinachoanza (first choice) umoja ukawepo ndani na nje ya mchezo ikiwemo’ jihad ‘ ya kuipambania timu yote haya yanawezekana

Mbinu za kisasa za kujihami ikiwemo formation ya kujipanga 4-5 -1 au 4-4-2 ama 3-5-2 zikiwa zimelenga kuwa na idadi kubwa ya walinzi mara wapotezapo mpira
Pasi fupifupi wakisogelean

Pamoja na yote namtanguliza mnyama hatua ya robo fainali huku tukitafuta ‘mgombea mwenza’

Sambaza....