Jonas mkude akimnyanyasa kiungo wa Al-Ahly
Blog

Simba kuishusha Al-Ahly nchini.

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imetuma ujumbe wake ukiongozwa na CEO mpya Barbar Gonzales na Mulamu Ng’hambi nchini Misri katika klabu ya Al-Ahly ili kuweza kuanzisha ushirikiano kwa klabu hizo mbili.

Mapema leo CEO wa Simba alikutana na uongozi wa Al-Ahly na kukubaliana kushirikiana katika nyanja mbalimbali za soka iliwemo katika miundombinu, ufundi pamoja na uongozi katika maswala ya soka.

Taarifa kutoka kwa klabu ya Simba imeeleza Al-Ahly wamekubali kushirikiana na Simba katika kujenga kituo cha kukuzia vijana cha soka, pia Alhly kuja nchini kucheza mchezo wa Kirafiki na Simbasc.

“Ofisa Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez akiongozana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi wametembelea makao makuu ya klabu ya Al Ahly yaliyopo jijini Cairo, Misri na kukubalina kushirikiana kwenye maeneo ya biashara, ufundi na uendelezaji wa wachezaji kwa kujenga kituo cha kukuza vipaji kwa ushirikiano na timu ya Al Ahly ikiwa ni kituo cha kwanza nje ya Misri (barani ya Afrika) ambacho kitaendeshwa na Simba na klabu hiyo.” Taarifa kutoka klabu ya Simba.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Mlamu Ng’hambi  (kushoto) Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez (kulia) wakimkabidhi jezi ya Simba kiongozi wa Al-Ahly (katikati).

“Pia wamekubaliana hapo baadae timu hiyo kuja nchini kucheza mchezo wa kirafiki na Simba SC.” Chanzo hicho kiliongeza.

Huenda katika Tamasha kubwa nchini la Simba Day mwakani Al-Ahly wakaalikwa nchini kuja kucheza mchezo wa Kirafiki na klabu ya Simba.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.