Ligi Kuu

Simba ni bora kuzidi sisi Alliance

Sambaza kwa marafiki....

Jana kulikuwa na mechi ya ligi kuu ya Tanzania bara ambayo ilikuwa ni kiporo kati ya Alliance na Simba ambayo ilichezwa katika uwanja wa CCM Kirumba.

Katika mechi hiyo Simba ilifanikiwa kushinda kwa goli 2-0 , magoli yaliyofungwa na Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Adam Salamba.

Baada ya mchezo huo kocha msaidizi wa Alliance Kessy Mziray amedai kuwa Simba ni bora kuzidi wao Alliance ndiyo maana wamepoteza.

“Ukitazama mchezaji mmoja mmoja Simba wana wachezaji ambao ni bora kuzidi sisi. Na wachezaji hao wamecheza katika mashindano ya kimataifa”.

” Tumezidiwa , kwa mchezaji mmoja mmoja wao walikuwa bora sana kuzidi sisi”.

Simba itapumzika kesho na kesho kutwa watakuwa na mechi dhidi ya KMC katika uwanja wa CCM Kirumba. Na baada ya mechi hiyo watasafiri kwenda katika mkoa wa Mara kucheza na Biashara United ya Mara.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.