Sambaza....

Timu ya SimbaSc iliyocheza mchezo wake wa ligi dhidi ya Njombe Mji na kupata ushindi wa mabao mbili kwa sifuri, inatarajiwa kuondoka asubuhii hii kuelekea Iringa.

Mchezo wao unaofwata wa ligi utakua ni Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani watakaoikaribisha SimbaSc utakaopigwa katika dimba la Jamuhuri Morogoro.

Kikosi cha Simba kitaweka kambi ya muda katika mji wa Iringa na kufanya mazoezi yake katika dimba la Samora. Ambapo itakaa Iringa mpaka siku ya Ijumaa na kuelekea Morogoro tayari kuwakabili Mtibwa Sugar.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na kiwango kizuri cha vijana wa Mtibwa Sugar pia na matokeo ya mechi ya raundi ya kwanza ambapo walitoka sare ya bao moja kwa moja, huku Simba wakisawazisha katika dakika dakika za nyongeza kupitia kwa Emmanuel Okwi baada ya bao la mapema la Stamil Mbonde kuipa uongozi Mtibwa Sugar.

 

Sambaza....