Sambaza....

Kuelekea mchezo wao wa pili wa klabu bingwa Africa katika kundi D dhidi ya AS Vita ya Congo klabu ya soka ya Simba leo imetoa taarifa rasmi kuhusu safari yao ya kuelekea nchini Congo DR.

Msemaji wa klabu ya Simba ndugu Hajji Manara amesema “Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi kadhaa wa klabu ya Simba utaondoka nchini kesho Alhamis ya tarehe 17January kwenda Kinshasah Congo kwenda kuwakabili Klabu ya AS Vita.”

Cleotas Chama

“Simba itaondoka asubui saa mbili na ndege ya shirika la ndege la Kenya kupitia Nairobi na kisha kuunganisha hadi Kinshasah Congo na itarejea Jumapili usiku na ndege hiyohiyo.” Manara pia aliongeza “Mchezo huo ni wa pili kwa Simba katika hatua ya makundi na unatatijiwa kuchezwa siku ya Jumamosi hii tarehe 19 saa 11 jioni kwa saa za Congo sawa na saa 1 jioni kwa saa za Tanzania.

Simba sc leo imefanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa Bokko Beach huku wakiwa tayari kabisa kwa safari. Nahodha wa timu hiyo John Bocco ndie mchezaji pekee mwenye hatihati ya kuukosa mchezo huo wa ugenini.

Sambaza....