Blog

Sipendi kuitwa Mbappe, namkubali Suarez

Sambaza....

Kelvin John amekiri mwenyewe kuwa hafurahishwi na mashabiki kumuita Mbappe, na angependa afahamike kama Kelvin yeye kama yeye. Mshambuliaji huyu ambaye ameng’ara na kikosi cha Serengeti Boys, ameitwa pia katika kikosi cha awali cha Taifa Stars. Fuatilia mahojiano kati ya Kandanda na Kelvin John hapa chini.


Kandanda : Mashabiki wanapenda sana kukuita Mbappe, huwa unajisikiaje ukiitwa Mbappe?

Kelvin John : Kwanza kabisa sipendi kuitwa Mbappe.

Kelvin John Kushoto

Kandanda: Kwanini hupendi kuitwa Mbappe?

Kelvin John : Kwa sababu kwanza kabisa Mbappe ni mchezaji mkubwa tumemuona amefanya vizuri kwenye mashindano ya kombe la dunia na anaendelea kufanya vizuri.

Pili, Mbappe ni mchezaji mkubwa sana sijamfikia alipo Mbappe, nashukuru sana kwa mashabiki kuniita Mbappe.

Kylian Mbappe

Na kuniona nacheza kama Mbappe lakini kwangu mimi sipendi kufananishwa na mtu ambaye sijamfikia kwa chochote kile.

Mimi napigana ili siku moja watu waniite Kelvin, ili mchezaji fulani afananishwe anavyocheza kama mimi, kwa hiyo sipigani kuwa Mbappe napigana kuwa Kelvin.

Kandanda : Ni mchezaji gani ambaye huwa unamfuatilia mara kwa mara?

Kelvin John : Namfuatilia Luiz Suarez .

Kandanda : Kwanini ?

Kelvin John : Kwa sababu napenda anavyocheza, anavyofungua kuomba mpira na anvyofunga.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.