EPL

Solskjaer: Henderson atakua kipa chaguo la kwanza.

Sambaza....

Kocha mkuu wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anasema Dean Henderson amethibitisha anaweza kuwa mlinda mlango namba moja kwa Man United na timu ya Taifa ya England.

Henderson ametumia misimu miwili iliyopita akiwa kwa mkopo kama kipa namba Sheffield United. Mlinda mlango huyo ambae ni zao la Man United Academy  alipanda na Sheffield United chini ya Chris Wilder huku akiendelea kufanya vizuri katika EPL na kupelekea klabu yake ya Sheffield United kua miongoni mwa timu tano za juu katika msimamo.

Dean Henderson akiokoa hatari katika lango lake akiitumikia Sheffield United.

Ole “Dean alifanya uchaguzi mzuri zaidi ya miaka sasa na amekuwa na maendeleo mazuri, tunaangalia hilo suala ambapo atakuwa wapi msimu ujao, lakini bado halijaamuliwa.”

“Msimu huu amethibitisha uzoefu mzuri kwake, amejionyesha uwezo wake, na amethibitisha kuwa ni kipa chaguo namba moja England na namba moja pia Man United  wakati fulani.”

Kwasasa lango la United lipo chini ya Muhispania David Degea ambae ametoka kusaini mkataba mpya wa miaka minne mwaka jana September. Shauku ya Ole kutaka kuona lango la United linakua chini ya Muingereza Henderson huenda likakutana na kikwazo cha kiwango cha David Degea kwasasa.

Sergio Romero ameshindwa kabisa kumpa changamoto Degea katika kuwania nafasi na hivyo kumfanya Degea kutamba katika milingoti ya mashetani wekundu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.