EPL

THIS IS ANFIELD” MINAMINO

Sambaza....

 

Na Emre Mursal Can

ilikua January 19,2018 mida ya saa 2:58 usiku , siku na muda huo nliandika makala iliyomuhusu “the little magician” Philippe coutinho , nilimwambia coutinho nenda ila ukae ukijua “YUPO ATAKAYEPOKEA ULIPOISHIA” baadae nilipokea pongezi nyingi Sana kuhusu makala ile na Kuna shabiki Mmoja alifika mbali zaidi na kutokwa machozi juu ya nilichokiandika. Na Kila nilichokiandika katika makala ile kwa Hakika kilitokea kwa asilimia Mia moja ndani ya jiji la Liverpool! Ni Kama vile niliichora ramani ya safari ya Liverpool baada ya coutinho.

Baada ya takribani mwaka Mmoja na miezi kadhaa kuiweka kalamu yangu chini bila kuandika chochote juu ya kiumbe yoyote wa Liverpool. Leo naja kwako MINAMINO, na ujumbe wangu wa Kwanza kwako ninakwambia “tupe Kila chembe ya nguvu,akili na uwezo wa mwili wako, tupe Kila kilichopo katika miguu yako, na sisi Kama Liverpool tutakufanya ujengewe sanamu Tokyo Japan”

Takumi, nakwambia sahau kuhusu majina makubwa yaliyopo anfield kwa Sasa na ujali thamani ya logo ya jogoo itakayokua kwenye moyo wako juu ya jezi ya Liverpool mwilini mwako, huku ukiweka akilini mwako kuwa anfield hakuna kiumbe Bora Zaidi ya Liverpool, hakuna star atakayekuwa na umaarufu kuliko jezi na logo ya Liverpool.

MINAMINO, anfield sio uwanja Ni nyumbani kwenu, Liverpool sio klabu Ni familia na sisi mashabiki sio washangiliaji Bali Ni ndugu zako! Leo nakwambia zile nyasi bandia za dimba la anfield hazikuwekwa mbolea ya mnyama au ya kiwandani Bali mwili wa Billy shankly ulichomwa Kisha majivu yake yalimwagwa juu ya nyasi hizo. Na ndio maana hakuna mpinzani Bora Zaidi ya Liverpool ndani ya anfield.

TAKUMI, ukiwa unatoka katika vyumba vya kubadilishia nguo kuelekea uwanjani kabla hujapiga hatua moja kushuka kwenye ngazi utakutana na kibao juu kimeandikwa “THIS IS ANFIELD” Ni lazima ukishike, na ile si ubishoo au staili Fulani ya manjonjo Bali Kuna “connection” iliopo Kati ya maneno Yale na Kila mpira au pasi itakayopigwa na mguu wa mchezaji yoyote wa Liverpool, sema tuu kipo juu ila kingekuwa chini basi Kila mchezaji angekigusa na mguu Wake kabla ya kuingia uwanjani. THIS IS ANFIELD.

MINAMINO, Liverpool ndio jiji pekee lenye thamani halisi ya mpira wa uingereza na ulaya kwa ujumla, anfield ndio pahala pekee kwenye vikombe vingi kuliko sehemu nyingine yoyote uingereza, anfield Kuna vikombe vipatavyo 47, anfield ndio uwanja pekee ambao jina lako litaimbwa kuliko unavotarajia na kufikiria.

TAKUMI, anfield ndio pahala pekee ambapo mwafrika anaweza kuwa Zaid ya mzungu, chukua mfano kwa mane na Salah, anfield ndio pahala pekee ambapo unaweza ukaenjoy kukaa hata bench au kucheza kwa dakika kumi tuu na bado muda mfupi baadae ukawa ni miongoni mwa wanasoka Bora zaidi katika kitabu Cha historia za ligi ya mabingwa ulaya chukua mfano kwa divock origi.

MINAMINO, nakukumbusha , kabla yako walikuepo kisuke Honda na shinji kagawa , lakini hao wote hawajawahi kuwekewa kumbukumbu yoyote katika nchi ya Japan, ila tunakuahidi “tupe Kila ulichonacho, na sisi Kama Liverpool tutakufanya ujengewe sanamu Tokyo Japan.

Klop (Kocha wa Liverpool)

Karibu nyumbani MINAMINO hapa ndipo mahala pekee ambapo vya kawaida huonekana Bora duniani , na kwa takwimu ulizonazo Salzburg ukizileta anfield Basi kwa Mara ya Kwanza tutashudia mchezaji mweny asili ya Asia anaingia katika kinyang’anyiro Cha ballon D’or na ukishndwa kachukua basi hata kumi Bora utakuepo! Njoo uwe sehemu ya historia ya kuchukua EPL baada ya miaka zaidi ya 20.
Njoo uendeleze alipoishia coutinho and I promise , YOU WILL NEVER WALK ALONE TAKUMI.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.