Stori

Tigana: Morrison ajue anaichezea Yanga!

Sambaza....

Wapwa, Mwana Mpotevu Karejea Nyumbani. Nitumie nafasi hii kumkumbusha bwana mdogo Benard Morrison, timu anayoichezea inaitwa Yanga Africa ina aina yake ya kujiheshimu kama mchezaji.

Ndani ya Club ina visa na mikasa ya kufukuza wachezaji bora kwa utovu wa nidhamu kuna kisa maridhawa cha Said Sued “Scud” kuwafunga Simba mara mbili ndani ya msimu moja na bado mwisho wa msimu wakamuacha. Si kwamba alishuka kiwango nidhamu yake ilielezewa si nzuri ndani ya Club.

Benard Morisson.

Lakini pia kuna mwaka Yanga ilisafisha timu kwa 75% sababu zaidi za kinidhamu na si za “kiperfomance”, usijiamini kwa mchango wako kwenye mechi ya watani wa jadi, ukaamini wewe ni kila kitu.

Kama una madai kaa mezani na waajiri wako meneja wako au wakala wako wasiishie kwenye kusaini mikataba tu lazima wawajibike pia kwenye madai yako. Hivyo kama una madai meza ya duara ni jawabu kaa chini tatua migogoro yako, kuingia mitini kuzima simu si ufumbuzi. Nasubiri kuona Yanga Afrika itatoa msimamo gani katika hili “otherwise” upande mwingine hatujausikia.

Sambaza....