Ligi Kuu

Tulitamani Singida Utd iwe Azam Fc, Azam Fc inatamani iwe Singida United

Sambaza....

Tumaini lilianza kujengeka mioyoni mwetu kwa sababu tuliona kuna kitu kinachoitwa “mbadala” katika mpira wetu.

Wengi wetu tumechoka na tunataka kuona mabadiliko makubwa yenye mwanga wa mafanikio katika mpira.

Ndiyo maana tunapoona mtu anakuja kama “mbadala” wa maendeleo ya mpira wetu humpenda na kumpa ushirikiano mkubwa huku tukimtia moyo aweze kufikia tunapopatamani.

Nafasi ya Singida Tano Bora

PosTimuPWDLGDPts
11881294316261430
21871254220193417
31901054936148364
4182546563-17227
5182556067-35225

Tunatamani sana tufike mbali kwenye mchezo huu tunaoupenda sana, tunatamani kuona timu kubwa za Taifa zikija hapa na kuondoka zikiwa na huzuni kutoka kwenye timu yetu ya Taifa.

>> Singida United, anzeni walipokosea Mbeya City

Tunatamani kuona TP Mazembe mpya katika ardhi yetu, ndiyo maana tulifurahi sana tulipowaona Azam FC wakija na uwekezaji mkubwa. Waliwekeza kwa kiasi kikubwa sana katika klabu.

Wachezaji wanao na walio ichezea Azam Fc

Klabu ya Azam FC ikawa na uwanja wake wa mazoezi pamoja na uwanja wa kuchezea mechi, hata wachezaji waliishi katika mazingira bora kwa sababu hosteli nzuri zilijengwa kwa ajili yao

Waliweka vitu vingi vya muhimu kwenye klabu, tukawa tunasubiri ni lini Azam FC itakuwa na uwezo wa kumtoa TP Mazembe katika michuano ya kimataifa.

Subira yetu haikuwa na kikomo, tuliamini ipi siku itatokea hivo hatukuchoka kusubiri. Wakati tukiwa tunasubiri Singida United masikio yetu yakasababisha macho yetu yaitazame Singida United kwa shauku.

Tuliona dalili za nafanikio mengine pia sehemu hii, dunia ya sasa mpira ni biashara. Biashara ambayo unaweza kutangaza bidhaa za mfanyabiashara na klabu ikanufaika.

Eneo hili halijawahi kutiwa mkazo katika mpira wetu, lakini Singida United walituonesha kuwa inawezekana kupata wadhamini kwenye mpira wetu kama utakuwa na uongozi wenye ushawishi nje ya uwanja.

Sportspesa, moja kati ya Wadhamini wa Singida Utd

Walionekana kuiendesha kibiashara timu, hawakusita kwenda na barua za maombi za kutaka udhamini sehemu mbalimbali, uoga wa kuwa ni timu changa iliyopanda daraja haukuwepo ndani yao.

Mikakati yao dhabiti juu ya uendeshaji wa klabu yao waliianisha kwenye barua za kuomba udhamini na waliwavutia wengi mpaka wakafanikiwa.

Mechi za Singida

TareheMwenyeji-Mgeni

Ile dhana ya kwamba wadhamini hupenda timu kubwa ikaondoka, tukabaki tukisubiri kipi kitafuata baada ya wadhamini

Ni mapema sana kutoa hitimisho kwa Singida United kwa sasa lakini ukweli ni kwamba walipoamua kufanyia ukarabati uwanja wa Namfua tuliamini wanafuata njia za Azam FC

Lakini hofu yangu ni moja, wanaweza wakawa wanapitia njia aliyotumia Azam FC lakini wakashindwa kujua kwanini njia ile haijafanikisha kuwafikisha Azam FC mbali?

Kikosi cha Singida

Azam FC wamewekeza sana kwenye klabu na kuisahau timu kitu hiki kinaonekana kwa Singida United. Mikakati yao mingi ni kuwekeza kwenye klabu na kuisahau timu.

Unaweza ukawa na kiwanja, Gym, Hostel, bwawa la kuogelea na wadhamani wengi kwenye timu lakini kama hujawekeza kwenye timu ni ngumu kupata mafanikio makubwa.

Timu haiishii kuwa na kocha wa kigeni na wachezaji wengi wa kigeni peke yake. Kuna maeneo mengi ambayo hatutaki kuyafikiria kuyawekeza kwenye timu.

Hatuna sporting director, director of football, scouts, wachambuzi wa kwenye timu. Ni watu muhimu kwenye timu lakini hawapewi kipaumbele kikubwa.

Ndiyo maana ni rahisi kwa timu kusajili mchezaji wa kiwango cha chini (awe kutoka ndani au nje ya nchi) kwa sababu timu hawana scouts wa kuwafuatilia wachezaji hawa kabla hawajasajiliwa ili kujua kama ana kiwango kinachokidhi mahitaji ya timu.

Hata kwenye mechi za kimataifa hatuna wachambuzi ambao hutumwa na timu kwenda kuangalia timu pinzani na kuja na uchambuzi wa uchezaji wa timu husika, mpira sasa hivi una uwekezaji mkubwa wa mbinu ndani ƴya uwanja unatakiwa uwe na watu wa aina kipindi mechi inapoendelea ili kusaidizana na benchi la ufundi kuona madhaifu ya timu husika kimbinu na kimfumo.

Tuliwaona Azam FC wakijenga hostel tukajua ni muda sahihi kwao wao kuwa na timu za vijana ili kuzalisha wachezaji watakaotumika katika timu ya wakubwa kwa baadaye au kuwauza kwenye timu zingine, lakini njia waliyopo Azam Fc inawarudisha kukutana na Singida United inapokuja sehemu ambayo Azam FC imekwama.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x