Kikosi cha Simba kikiwa mazoezini
Blog

Ujumbe wa Simba ulio mchungu kuumeza!

Sambaza....

Haloo!! Ndugu kutoka Msimbazi, waite majirani na wanamichezo wote wa Simba kisha weka ‘Loudspeakers’ hii simu ya mwandishi wa kushoto wasikie nachonena.

Mimi ni mjumbe tu niliyetumwa na wafuasi wengi wa soka na mashabiki wa klabu hio Simba. Ikumbukwe mjumbe hauwawi.

Sajili za Simba nimeziona zina tija kubwa katika kutengeneza kikosi kipana chenye ushindani pia kujenga morali ya timu.

Bwalya, Mugalu, Mkude na Morisson.

Tambueni kuwa raha ya mpira uchezwe, bila kupepesa macho naiona safu ya ulinzi kukiwa na wachezaji wasiopungua 9. Ame na Kennedy wapeni muda wafanye “Rotation” mbele ya wakongwe Nyoni, Wawa na Onyango, hizo ni silaha zenu baadae bila kusahau Fred Kameta “Duchu” na Gadiel Michael wapeni nafasi pia mechi ni nyingi.

Fraga na Mkude hakuna matata, Ndemla huyu maamuzi atafanya mwenyewe maana wajumbe wanasema walishamshauri sana, Shiboub nasikia anaondoka, sawa.

Jonas Gerald Mkude “Nungunungu”

Juu hapo kuna Wazambia wawili, Chama na mdogo wake mpya Bwalya, hakuna shaka, vipi Mzamiru wapi ataenda? Mtafutieni timu. Dilunga na Miraji, waacheni wapambanie namba lakini Kichuya, Ajibu na bwanamdogo Rashid wakopeshe timu zanazowahitaji, Deo Kanda nadhani akiondoka sawa tu.

Kahata, Miquissone na Morisson, kazi imeisha, mabega yenu (Simba) yapo sehemu salama hawa waacheni wale utawala.

Ibrahim Ame

“Kijiji bila wazee ni uhuni” hii kauli inatafsiri safu ya ushambuliaji ya Simba, Kagere, Mugalu na Bocco kazi wanaiweza, ombi la wajumbe ni kumpa nafasi kijana Nyati Charles Ilamfya hata robo ya michezo ya Simba ili afanye kitu huku akijifunza mbele ya miamba hio pasi kumsahau bwana mdogo Cyprian Kipenye nae mpeni muda acheze mechi ni nyingi.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.