La Liga

Usiteleze ukiwa dunia ya Ronaldo, Usianguke ukiwa dunia ya Messi

Sambaza....

Ureno na Argentina ndizo nchi ambazo kwa sasa zinaonekana zinamiliki wafalme wa soka duniani.

Wafalme ambao wamefanikiwa kujenga nguzo imara katika falme zao.

Nguzo ambazo zinaonekana ngumu kwa kizazi kinachokuja kuzivunja, inawezekana mikono yao hawa watu wawili ilikuwa dhabiti kwenye ujenzi wa nguzo hizi.

Ujenzi ambao umefanyika kwenye mashindano mengi ambayo miguu yao ilikanyaga.

Miguu yao ilifanikiwa kufanya maajabu kwenye michuano ya klabu bingwa barani ulaya ndiyo maana Cristiano Ronaldo amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa wakati wote katika michuano hii akiwa na magoli 119

Lionel Messi hakuingiwa na wivu ndani ya moyo wake alichokifanya ni kuwekeza nguvu kwenye ligi kuu ya Hispania , La Liga na kuwa mfungaji bora wa wakati wote wa La Liga akiwa na magoli 374 huku Cristiano Ronaldi akiwa na magoli 303

Hii yote inaonesha hawa watu wapo katika dunia zao za peke yao, dunia ambazo unatakiwa ufurahie kuziishi kwa sababu hakuna kizuri unachoweza kukosa kati ya hizi dunia mbili.

Dunia ambazo zimeundwa kwa maumbo tofauti tena na watu wenye ujuzi tofauti. Kuna watu wawili wamehusika kuunda dunia hizi mbili.

Msanii ni mtu wa kwanza aliyetumia muda wake mwingi kuunda dunia yake ambayo aliona inafaa kutoka na mafikirio yake.

Aliweka vitu vingi kwenye dunia yake, naksi nyingi zilihusika ili kupendezesha dunia hii, nakshi ambazo zilimwezesha kumpata mtu mwenye uwezo mkubwa wa kukokota mpira , kupiga vyenga na sanaa zingine nyingi, mtu huyu ni Lionel Messi.

Mtu ambaye anatofautiana kubwa ambaye ni Cristiano Ronaldo. Mhandisi ndiye mtu aliyetumia muda wake kumuumba mtu huyu.

Cristiano Ronaldo

Alitumia nguvu na akili nyingi kuhakikisha anapata mtu ambaye ana uwezo wa kufanya kazi kwa bidii bila kuchoka tena kwa kiwango kikubwa kama mashine, akafanikiwa kupata mtu ambaye anauwezo mkubwa wa kufunga magoli kwa wingi.

Sanaa aliiweka ndani ya mwili wa huyu mtu, lakini sanaa yake ilikuwa ya muda mfupi kiasi kwamba kadri muda ulivyokuwa unazidi kwenda ndivyo hivo sanaa ilikuwa inapungua miguuni mwake lakini magoli yakawa yanaongezeka katika miguu yake, ndipo hapo tukampata Cristiano Ronaldo.

Binadamu kwenye hat tricks 50 mpaka sasa hivi, hat tricks zinazonesha kuwa yeye ni muhimu zaidi kwenye kila timu aliyocheza katika maisha yake kama alivyo Lionel Messi.

Umuhimu wao ni mkubwa sana katika kuamua matokeo kutokana na uwezo wao binafsi, hakuna kigumu kinachoshindikana kipindi Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wanapokuwa uwanjani.

Lionel Messi

Unatakiwa uwe na imani kuwa lolote linaweza kutokea kwa sababu yupo Criastiano Ronaldo na Lionel Messi, watu ambao ni timu waliopo ndani ya timu.

Kama ilivyo kwa Barcelona ilivyo na timu mbili yani Barcelona yenyewe na Lionel Messi , ndivyo hivo ilivyo kwa Real Madrid wanatimu mbili pia ambazo ni Cristiano Ronaldo na Real Madrid.

Hii ni mihimili mikubwa sana katika mpira na timu zao, washindi mara tano kila mmoja wa Ballon D’or.

Hutakiwi kujitesa kuchagua kuishi dunia moja pekee na kuichukia dunia nyingine, kama utaamua kuwa dunia ya Lionel Messi unatakiwa ufurahie kuona ustawi wa dunia ya Cristiano Ronaldo.

Kuwepo kwako katika dunia ya Cristiano Ronaldo kusifanye ukuze chuki kwenye dunia ya Lionel Messi.

Kuwekeza chuki katika ya dunia ambayo wewe hauishi hakukusaidii chochote , unachotakiwa kufurahia kumuona anachokifanya Lionel Messi huku mapenzi yako yakibaki kwa Cristiano Ronaldo.

Mapenzi yako yasikutie upovu na kuacha kuona kizuri anachokifanya mpinzani wako, hawa ni wachezaji bora kwa sasa na wamedumisha kiwango chao kwa miaka 10 mfululizo bila kushuka

Wameshinda tunzo nyingi binafsi, wakashinda makombe mengi huku wakivunja na kuweka rekodi mpya ambazo unatakiwa ujivunie kuzishuhudia zikiwekwa na miamba hii miwili

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x