Sambaza....

Muda huu kelele za pesa hazisikiki kwa kiasi kikubwa kama ilivyokuwa awali, mategemeo yetu yalikuwa makubwa sana baada ya kuamua kutumia pesa nyingi kununua pasi za mwisho, magoli na uwezo wa kukaba na kushambulia.

Tuliamini pesa zimeleta mtu ambaye angekuwa na uwezo wa kusimama na kuonekana kama nembo kubwa ya klabu.

Kila jicho ambalo lilikuwa linatazama uwanja wa Old Trafford lilianza kuona kwa mbali Paul Pogba kama ndiye nembo kubwa ijayo ya timu.

Pengine umri wake ulikuwa unamruhusu kujenga nembo imara kwenye timu ya Manchester United, na pengine uwezo wake mkubwa aliouonesha katika timu ya Juventus kabla hajaja Manchester United ndiyo ulitia matumaini makubwa kuwa Paul Pogba ndiye mfalme ajaye ndani ya kikosi cha Mnachester United.

Image result for paul pogba images

Tena alikuja wakati mzuri kwake, wakati ambao milango ya Old Trafford ilikuwa tayari kufunguka kwa ajili ya kuweka njia ya kutokea kwa Wayne Rooney, njia ambayo aliitumia Paul Pogba kuingia.

Lilikuwa jambo zuri na ilikuwa vyepesi kwake kuweka jina lake ndani ya mioyo ya mashabiki wa Manchester United kwa sababu Mfalme Wayne Rooney alikuwa anamaliza muda wake wa Utawala pale Manchester United.

Mioyo ya wengi ilitamani mtawala ajaye angekuwa Paul Pogba kwa sababu ya pesa zilizotumika kumleta pale Old Trafford, pesa ambazo zilikuwa deni kubwa.

Msimu wa pili sasa huu unaelekea kuisha tangu pesa zimfanye Paul Pogba akanyage nyasi za viwanja vya Old Trafford, maendeleo yake yanakatisha tamaa mpaka sasa.

Wengi wameanza kupoteza imani na tumaini walilokuwa nalo kipindi ambacho Paul Pogba alipokuwa anakuja katika timu ya Manchester United.

Matumaini ya kuona Paul Pogba akifunga magoli ambayo yangeisaidia timu kupata mafanikio makubwa yameanza kupotea taratibu.

Image result for pogba and mctominay images

Hata imani ya wengi ya kutamani kuona Manchester United ikipata mafanikio makubwa kupitia nguvu na kivuli cha Paul Pogba imeanza kupotea.

Watu wengi wanatamani nyakati zile zilizokuwa na majira ya Juventus ndani ya maisha ya Paul Pogba zijirudie lakini ndivyo hivo upepo umekuwa mkali sana kwa Paul Pogba.

Umekuwa upepo wenye nguvu kubwa sana, tena kibaya zaidi ni upepo wa mawe na unavuma kuelekea kwenye uso wa Paul Pogba, muda huu ana kazi moja tu kubwa nayo ni kutumia mikono yake kujikinga uso wake dhidi ya upepo.

Hana kazi nyingine ya ziada kitu ambacho kimesababisha hata kocha wa Manchester United kutoendelea kumwamini kwa muda huu na imani yake kuielekeza kwa kijana mdogo sana Scott McTominay.

Image result for scott mctominay images

Viatu vyake vinaonekana vimebeba mahitaji muhimu anayoyataka Jose Mourinho. Ndiyo maana ikawa virahisi kwa Jose Mourinho kutumia viatu vya Scott McTominay kuficha pesa za Paul Pogba.

Ghafla anaonekana kutokuamini kuhusu nguvu ya pesa, hili ni jambo geni sana kwa Jose Mourinho ambaye tangu tumfahamu kwenye tasnia hii ya ukocha tumemfahamu kama kocha anayeamini pesa ina nguvu ya kuleta ushindi na makombe ndani ya timu

Muda huu akaonekana Jose Mourinho asiyekuwa mvumilivu na pesa, hakutaka kukaa na kuendelea kusubiri pesa zitakuja kumletea magoli na pasi za mwisho alichokifanya ni kugeuka upande wa pili na kumchukua Scott McTominay.

Akaweka imani kubwa juu yake, kitu kizuri alipoaminiwa kijana wa watu hakuonesha kumwangusha kocha wake aliyemwamini, akawa anafanya kitu kulingana na alichokuwa ameagizwa kufanywa na kocha.

Huu ndiyo msingi wa Jose Mourinho kila anapopita, hutaka kuona mchezaji akifanya vitu vingi anavyomwagiza mchezaji ndani ya uwanja.

Image result for scott mctominay images

Alipokuwa anatakiwa kukaba alikuwa anakaba kweli na hii ndiyo furaha ya Jose Mourinho kuwa na timu inayokaba sana.

Alipotakiwa kuipandisha timu alifanya kama alivyoelekezwa kwa kiwango kikubwa na utulivu mkubwa ndani yake na hakutengeneza uwazi mkubwa kati yake na Nemanja Matic katika eneo la katikati mwa uwanja.

Ukomavu mkubwa ukawa unaonekana ndani yake , akawa anafanya maamuzi ya kikubwa tofauti na umri wake, alifikia hatua mpaka hatua ya kuilisha familia yake bila kujali umri aliokuwa nao , kikubwa nidhamu ilimuongoza.

Nidhamu ambayo ilimfanya atimize jukumu lake ipasavyo uwanjani. Ikawa kawaida kumuona Paul Pogba akianzia benchi ndani ya michezo minne.

Hata lawama za kwanini Paul Pogba haanzi zilipungua kwa sababu thamani ya pesa ya Paul Pogba ilionekana ndani ya kiatu cha Scott McTominay.

Sambaza....