Viongozi wa Yanga na GSM katika hafla ya utiaji saini ya uhusiano na Laligaga
Blog

Viongozi Yanga wanacheza na akili zetu?

Sambaza....

Yanga hii inabahatisha sana na inacheza na “mindset”zetu mashabiki. Yanga ya MANJI inabaki kuwa bora sana kwangu na wala haikuwa na tension kwenye usajili mitandaoni.

Ilileta watu kimya kimya na ikawatambulisha kwa mashabiki.  Kama tusipoenda kwenye mabadiliko hawa GSM watatutesa sana mashabiki na kubaki na maumivu ya La Liga na mkataba wenye Sevilla ndani yake.

Viongozi wa Yanga, Laliga na Mh. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

Sarakasi za Senzo zimeishia wapi kwetu Jangwani?
Ligi inaanza tarehe 06 September timu inafanya mazoezi kama ya Ndondo Cup haina hata Mwalimu Mkuu wala Msaidizi.

Anyway kiwanja cha Makonda kule Kigamboni bado tunafanya upembuzi yakinifu au kuna mkandarasi yupo site.  Watu waliominiwa na kupewa nafasi kwenye club yenye brand kubwa wanashindana kupost utumbo mitandaoni kwa kuwadanganya mashabiki.

Mashabiki wa Yanga!

Ngoja niwape kichekesho cha mwisho nendeni kwenye page ya Yanga kule Instagram muangalie kwanini waliiondoa picha ya mshambuliaji wa Ghana ambaye tulijulishwa amesajiliwa??

Napumzika na akili za w’kend hizi.

Junior Matukuta
Mbeya, Tanzania


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.