Sambaza....

Kivumbi cha Ligi Kuu Tanzania bara, kitaendelea tena ijumaa hii baada ya mapumziko ya takribani majuma mawili kupisha michuano ya kimataifa.

Ligi kuu hii licha ya changamoto za hapa na pale, imepata mwamko mkubwa katika kile tunaita, kupigania ushindi. Kwanza, Timu mbili zinatafuta kuwakilisha Taifa katika michuano ya kimataifa, Pili Timu moja inatafuta ubingwa ligi Kuu Tanzania bara pia kuna mafanikio binafsi na ya kitimu yakitafutwa.

Kwa upande wa mafanikio kitimu, timu zinatafuta ‘perfomance’ nzuri, ili kubaki katika ligi, na kwa upande wa wachezaji wanatafuta nafasi ya kuonekana ili wapige hatua katika maisha yao ya kandanda.

Tovuti yetu katika kutambua hayo yote, tunaendelea kuwapa motisha wachezaji kadri ya uwezo wetu ili kufanikisha malengo yao, na tumeaanza kwa kuwatambua wale wanaofunga mabao mengi ndani ya mwezi mmoja. Nani kuibuka kidedea mwezi huu baada ya David Ambokile Eliud mwezi uliopita? endelea kufuatilia tovuti hii.

Sambaza....