Tahariri

Waamuzi wa Soka Wanahitaji Kujengewa Uwezo si Lawama.

Sambaza....

Zimwi likujualo halikuli  ukakwisha, lakini hapa ni kinyume tunaangamia kwa kuliwa mpaka kwisha kwa zimwi litujualo.

Marefa wa Tanzania wamekua gumzo kwa muda mrefu sasa, sio msimbao au mshangao tena bali ni kawaida kwa sasa kwani imekua ni kada kwa waamuzi kuchezesha mechi chini ya kiwango, wamekua wakirudia makosa yale yale kila uchwao hakuna mabadiliko.

Tangia hapo sheria hufasiriwa tofauti wakati mwingine na mara nyingi kuna ukinzani wa kimaamuzi, waamuzi dhidi ya sheria wanazozisimamia na kuzifasiri.

Nini kinawakumba marefa ? Nini kifanyike?

Maslahi, kumekua na fununu na kashfa ya upangaji matokeo kwani baadhi ya marefa walionekana kuchezesha kwa upendeleo hususani timu kubwa zinapocheza na timu ndogo matukio tata hua ni mengi sana.

Hii inatokana na maslahi kiduchu wanayopokea hii inawafanya iwe rahisi kushawishika na baadhi ya ofa wanazokutana nazo hususani za kupanga matokeo kwani hata waamuzi pia wanafamilia zinazowategemea na wanahitaji kujijenga kiuchumi hivyo Shirikisho linalohusika liboreshe maslahi ya waamuzi ili waridhike na vipato watakavyopata.

Mapumziko, ili akili ya mwanadamu ifanye kazi vizuri inahitaji utulivu na utimamu wa mwili, utulivu wa kiakili humfanya mtu kufanya maamuzi sahihi. Inaonekana baadhi ya waamuzi wametumika kwa mda mrefu mfululizo huku wakipata mapumziko kiduchu hivyo husababisha fatiki na kuwafanya washindwe kufasili sheria vema badala yake wanafasili kichovu hivyo wapewe mapumziko. Mwamuzi achezeshe mchezo mmja au miwili kwa juma.

Mwamuzi Ramadhani Kayoko akisimamia mchezo kati ya Yanga na Zanaco ya Zambia.

Kozi za uamuzi, je kozi za waamuzi zinazotolewa nchini zina kidhi vigezo vya kimataifa? Je wahitimu wanakua tayari kutumika ipasavyo? Tumetoa marefa wangapi kwenda nje kuchezesha mashindano makubwa ama vile Afcon na World Cup? Jibu ni hakuna.

Basi TFF wapitie upya miswada ya kozi za marefa ili tupate waamuzi bora ambao wamefuzu kikamilifu katika kusimamia na kufasiri sheria za soka.

Nb: ukiona vya elea ujue vimeundwa


Sambaza....