Sambaza....

Baada ya kupoteza mchezo wa ugenini kwa mabao mawili kwa moja ugenini dhidi ya Nkana Rangers ya Zambia Simba inarudi katika uwanja wake wa nyumbani kujiuliza.

Klabu ya soka ya Simba inahitaji ushindi wa bao moja tu ili iweze kufuzu katika hatua ya makundi katika klabu bingwa Africa. Ikumbukwe goli lolote watakalopata timu ya Nkana katika mchezo wa marudiano  uwanja wa Taifa 

Haji Manara alisema “Tumeongea na wachezaji juu ya umuhimu wa hii mechi na uzito wake kwa simba na taifa kwa ujumla. Tumewaomba wapambane ili waweze kuandika historia katika soka la nchi yetu.

Manara aliongeza “Kwa kikosi chetu tunaamini tunaweza kufikia malengo yetu tuliojiwekea ya kuchukua ubingwa wa Ligi kuu bara na kufika makundi. Na katika makundi lolote linaweza kutokea, maana kuna point 9 za uwanja wa nyumbani halafu unatafuta suluhu moja away tayari unapata nafasi ya kusonga mbele”

Simba inatafuta rekodi ya mwaka 2003 baada kuitoa Zamalek ugenini. Tangu mwaka huo mpaka sasa ni miaka 13 imepita bila ya Tanzania kupata mwakilishi katika hatua ya makundi klabu bingwa Africa. Hata Yanga wamekua wakijitutumua lakini wameishia katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Sambaza....