Emmanul Okwi
Mabingwa Afrika

Wachezaji Simba waondoka, mastar kibao wameachwa.

Sambaza....

Kikosi cha wachezaji 20 kimeondoka jioni ya leo kuelekea nchini Algeria katika mchezo wake wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika kundi D huku baadhi ya wachezaji muhimu wakiachwa Dar.

Wachezaji 20 wa Simba pamoja na benchi la ufundi wameondoka leo na shirika la ndege  Fly Emirates wakipitia Dubai- U.A.E na kisha kuunganisha ndege ya kuelekea  nchini Algeria.

Kikosi kilichoondoka ni Aishi Manula, Deo Munishi, Zana Coulibaly, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Mohammed Hussein, Pascal Wawa, Poul Bukaba, James Kotei, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Cletus Chama, Rashid Juma, Haruna Niyonzima, Abdul Selemani,John Bocco, Maddie Kagere,  Mohammed Ibrahim na Adam Salamba.

Baadhi ya wachezaji muhimu wakiwa wamebaki Dar kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo majeruhi na adhabu. Wachezaji wa Simba waliobaki Dar ni pamoja na Said Ndemla, Juuko Mursheed, Emmanuel Okwi, Erasto Nyoni na Ally Salim.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x