Ligi

Wachezaji watano wa SIMBA watakaouia YANGA

Sambaza....

Kesho ndiyo mechi ya watani wa jadi , mechi ambayo tutashuhudia nyasi za uwanja wa Taifa zikiwa moto . Timu zote katika mechi nne zilizopita hazijaruhusu hata goli moja, huku Yanga ikishinda mechi tatu na kutoka Suluhu mechi moja, huku Simba ikishinda mechi zote nne. Wafuatao ni wachezaji hatari zaidi wa Simba ambao wataiua Yanga.

HASSAN DILUNGA

Kuumia kwa Miraji Athuman kumempa nafasi ya yeye kuwa anacheza katika kikosi cha kwanza kwenye mechi za hivi karibuni. Ameimarika kwa sasa , anajua kuiunganisha timu kwa pasi zake pia anajua kutumia nafasi vizuri . Katika mechi nne zilizopita za Simba amefanikiwa kufunga magoli 2.


2 - 2
Uwanja wa Mkapa

Simba SC vs Yanga SC


MEDDIE KAGERE

Mwezi wa kumi na mbili umeisha kwa yeye kuendelea kuwa na goli moja tu. Kitu ambacho kimewashtua wengi , siyo kawaida kwa Meddie Kagere kumaliza mwezi akiwa na goli moja. Mechi ya mwisho iliyowakutanisha Yanga na Simba , yeye ndiye aliyefunga bao pekee la ushindi. Anabaki kuwa mshambuliaji hatari ambaye anaweza kuifunga Yanga wakati wowote.

DEO KANDA

Wakati anakuja kwenye kikosi cha Simba ilikuwa ngumu kwake moja kwa moja kuanza kung’aa, lakini hivi karibuni amekuwa na kiwango kizuri sana na yuko kwenye fomu nzuri , mechi nne zilizopita za Simba amefanikiwa kufunga magoli 2 na kutoka pasi ya mwisho ya goli moja. Amekuwa na msaada mkubwa Kwenye timu , kwa sasa yuko kwenye kiwango kikubwa ambacho kinaweza kuleta madhara kwa Yanga.

FRANCIS KAHATA

Yule Kahata wa Gormahia ndiyo huyu ambaye ameng’ara sana kwenye kikosi cha Simba kwa mwezi wa kumi na mbili. Anauanza mwezi wa kwanza yuko kwenye fomu na mechi yake ya kwanza kwenye mwezi wa kwanza ni dhidi ya Yanga , inawezekana Yanga wakawa na bahati mbaya sana kuhusiana na hili.

GERSON FRAGA

Msimu uliopita Simba ilikuwa na Double Pivot kati ya Jonas Mkude na James Kotei , lakini msimu huu inaonekana Simba hawana sababu ya kutumia Double Pivot tena Kwa sababu Gerson Fraga anaweza kucheza yeye kama yeye katika eneo la kiungo cha kuzuia, anawalinda vyema mabeki na anapeleka mipira vizuri kwenda mbele kwa pasi nzuri na Kibaya zaidi kwa Yanga anajua kufunga.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x